Elections 2010 Kuharibu kura

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
54,762
Reaction score
59,204
Asalam aleikum wanajamvi
jamani kuna jambo linanitatiza na natumai kila mtu anachangia kile anachokijua kuhusu hili,
ni hivi.wapiga kura wote ni watu wazima wanaojielewa hivi inakuaje mtu kapanga foleni kwa mda wa masaa mengi halafu at the end of the day unakuta kaharibu kura yake? Naongelea chaguzi zilizopita na inawezekana na mwaka huu kama kawaida kutakuwepo na kura zitakazoharibika,sasa hawa wanaoharibu kura ni kwamba wanajikomoa au ni tabia au ni kitu gani hasa kinapelekea?? Ahsanteni.
 
Na si ajabu nyingi ya kura zinazoharibika wahusika walikuwa wanakusudia kupiga kwa chama pinzani hivyo kasoro kidogo tu basi chama filisi cha mafisadi huzishupalia ili zisihesabike.
 
Na si ajabu nyingi ya kura zinazoharibika wahusika walikuwa wanakusudia kupiga kwa chama pinzani hivyo kasoro kidogo tu basi chama filisi cha mafisadi huzishupalia ili zisihesabike.

hili nalo neno. Kwa hiyo unaweza kuta kura ya chama pinzani ina kadoa kadogo tu ka wino basi wanakuambia imeharibika. Lakini za kwao hata uchore mtu ilimradi uliweka tiki kwao watakuambia period hesabu hiyo. Duh! Chama mufilisi.
 
hata uchaguzi wa papa kura zinaharibika
 
Ni Muhimu sana Vyama vya upinzania vikaweka msimamo sasa hivikuhusu namna ya kura zitakavyohesabiwa................teknolojia ya UWAZI kutoka kila kituo inahitajika.............hili jambo linawezekana kabisa kulidhibiti............
 
Eti alama ya vema ikigusa au itoka nje ya kisanduku basi kura imeharibika! Wakati si watanzania wote wanaweza kuandika kwa ufasaha.
 
Eti alama ya vema ikigusa au itoka nje ya kisanduku basi kura imeharibika! Wakati si watanzania wote wanaweza kuandika kwa ufasaha.

hii, ni kweli kabisa, ila wadau kinachotakiwa sasa hivi tuanze kuwaelimisha ndugu zetu, jinsi ya kupiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…