Kuheshimu katiba ni jukumu la kila raia. Malisa GJ na Joel Nanauka ni wahanga wa hili

Kuheshimu katiba ni jukumu la kila raia. Malisa GJ na Joel Nanauka ni wahanga wa hili

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Ninaandika huu uzi nikiwa nimekwazwa sana na baadhi ya watanzania wenzetu wasiojali katiba inavyosema kuhusu uhuru wa watu wengine. Kumekuwa na uvunjaji mkubwa wa sheria kwa sisi wananchi wa kawaida na tukibanwa tunasingizia viongozi.

Juzi kijana Joel Nanauka alipost kuomba kura za wajumbe kwenye uchaguzi wa wajumbe wa NEC CCM ila katika hali ya kushangaza alishambuliwa na wengi kwa kuonekana msaliti. Hoja ni kwamba hakupaswa kujihusisha na siasa kwasababu ya kazi yake ya kuhamasisha mambo ya ujasiriamali na kuwatia moyo watu wanaopitia changamoto mbalimbali. Baadhi wanadai kwanini ajiunge na watesi wao? Nikashangaa sana. Kama mtu anakutesa zipo taratibu za kisheria kupambana nae na sio kumbebesha mzigo Nanauka.

Wakati naendelea kutafakari ya Joel nikaona Malisa GJ wa CHADEMA nae akitoa tamko kwamba asiingiliwe kwenye kutoa maoni yake ya kisiasa na michezo kwasababu tu anajishughulisha kuchangisha michango ya kusaidia watu mbalimbali wenye shida hasa wagonjwa. Kuna baadhi ya wapumbavu wanadai maoni yake ya kisiasa na michezo vitasababisha watu wasichange. Yaani ujinga mtupu kuingilia uhuru wa kijana huyu muhimu kwa taifa.

Ninawasihi watanzania wenzangu tujitahidi kuheshimu katiba kwenye uhuru wa kutoa maoni na mitazamo ya kisiasa. Kama Nanauka anapenda CCM basi aachwe awe huru. Kama Malisa naye ni mfuasi wa Chama Cha Mbowe basi aachwe huru kuamini anachoamini bila bugudha. Na sio hivyo tu, hata wale wakikamata mwizi wanakimbilia kumuua waache.. wafuate sheria inavyotaka. Tukiweza kufuata sheria sisi kwanza basi tutakuwa na ujasiri wa kuwanyooshea vidole viongozi. Wewe mzazi unayemwona mwanao mjinga na mzembe kisa hali rushwa wala kujihusisha na dili kwenye ofisi za umma pia ubadilike.
 
Hakuna katiba yoyote iliyovunjwa kwa huyo mNanauka wako kuonekana hana maana.
Malisa umemuunganisha tu ili kutembelea nyota yake.
Zaidi sana ni raia wametimiza haki yao ya katiba kwa kutoa maoni yao kuwakosa.
 
Hakuna katiba yoyote iliyovunjwa kwa huyo mNanauka wako kuonekana hana maana.
Malisa umemuunganisha tu ili kutembelea nyota yake.
Zaidi sana ni raia wametimiza haki yao ya katiba kwa kutoa maoni yao kuwakosa.
Kuwa na nidhamu
 
Back
Top Bottom