Kuhudhuria semina/training mameneja badala ya maofisa

Kuhudhuria semina/training mameneja badala ya maofisa

walitola

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2014
Posts
4,796
Reaction score
5,553
Habari za asubui ndugu zangu, natumai wote muwazima wa afya.

Niende kwenye mada husika moja kwa moja, kumekuwa na tabia ambayo sio nzuri kwenye ofisi zetu unakuta imekuja safari labda kuhudhuria training/semina na kwenye hiyo semina utakuta inawataka waende maofisa sasa kutokana na roho za ubinafsi unakuta wakuu wa idara wanakwenda kwenye hizo semina na wakati mwingine zinakuja semina za mameneja pia nao wanataka kwenda sasa nashindwa kuelewa tunakuwa na roho mbaya kiasi hichi hivi kweli tutafika kwa staili hii kweli.

Hizi semina zinakuwa zinatoa mchango mkubwa sana kwenye kuongeza ufanisi hasa kwenye majukumu yetu ya kila siku sasa inakuwaje hawa ndugu zetu wanakuwa na urafiki kiasi hichi wizara zenye dhamana wanajua haya maovu yanayotendeka kweli au hawajui.

Naomba niwasilishe wadau
 
Kikubwa ni kupambana na wewe uwe mkuu wa kitengo ili uhudhurie semina na training. Kulalamika hakusaidii.

Maana Tanzania ya sasa sio ya Ujamaa tena. Kila mtu anaangalia tumbo lake na familia yake sio ustawi wa taasisi au shirika.

Chanzo cha yote ni wanasiasa kujilipa marupurupu kwa kisingizio cha kuwawakilisha wananchi.
 
Hata wewe ukija kua mkuu wa idara utakua unaenda semina zote mwenyewe yaani mkeo atakua anakuja stendi na begi la nguo safi unampa la nguo chafu aende nalo nyumban. Hakuna anayetosheka na pesa mkuuu
 
Mkuu ni kweli upo sahihi kabisa lakini kuna mda tuwe waungwana kwenye hili inakuja semina mtu wa chini kabisa inatakiwa akaudhurie labda afisa msaidizi badala yake anaenda meneja wa idara husika apa inakuwa haijakaa sawa kabisa.
 
Hata wewe ukija kua mkuu wa idara utakua unaenda semina zote mwenyewe yaani mkeo atakua anakuja stendi na begi la nguo safi unampa la nguo chafu aende nalo nyumban. Hakuna anayetosheka na pesa mkuuu
Kiongozi siwezi kuwa na roho ngumu kama hiyo hata kama nitakuwa bosi hizi pesa zisikuondolee utu na ubinadamu
 
Back
Top Bottom