Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,053
- 2,207
Tanzania ipo katika mchakato wa kuandaa mashindano makubwa ya AFCON Mwezi Julai 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.
Tukio hili ni la kipekee na limetumia rasilimali nyingi hadi sasa na pia ni tukio la kimanufaa linalotamaniwa na kila nchi Africa.
Hadi sasa kwa muelekeo wa kimazingira Tanzania ipo mbele katika hatua za maandalizi yaani ukiangazia uwepo wa viwanja,mashabiki na huduma zinazokidhi kuandaa mashindano haya makubwa.
Soma Pia: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
Katika miaka mitatu ya hivi karibuni Tanzania imeonesha uwezo kupitia timu zake,ligi yake na ushindani wa kimataifa katika soka barani Afrika kulinganisha na miaka zaidi ya 40 iliyopita.
Zaidi Tanzania imekuza diplomasia katika soka kwa kiasi kikubwa.
Naamini jambo hili haliwezi kuwapendeza mataifa mengine yasiyoitakia mema nchi yetu.
Kwa muktadha huu lazima kila tukio liache maswali na maswala ya kufanyia kazi kwani soka ni uchumi,diplomasia au vita baridi.
Tukio haribifu dhidi ya dabi kubwa Afrika kwa sasa yaani kati ya Simba na Yanga ni tukio linalohitaji uchunguzi wa kina sana...
Ni vyema uchunguzi huo ukafanyika kwa kina na matokeo yakafanyiwa kazi haraka.
Kwa upendo wa nchi