Sehemu chache nchini na hasa za mijini zimepata elimu ya sheria ya mabadiliko ya katiba, maeneo mengi bado, waliopata wanataka kuijua katiba iliyopo walinganishe waamue. Mashirika ya hiari yamejitahidi kutoa elimu na bado haitoshi, nguvu na juhudi za ziada zinahitajika. Kuna tija nadhani kwa vyama vya siasa kuchangia na kuwakilishwa kwa sababu wafuasi wao ni raia wenye haki kuwakilishwa katika jambo hili. Kimsingi hakuna kundi la jamii lisilotakiwa kuwakilishwa mambo ya katiba.