Kuhusu ABC Bank

mtanzania10

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
271
Reaction score
81
Ndugu wana jamvi hii benki tajwa hapo juu imekuwa na matawi mengi nchi nzima. lakini katika wilaya nyingi wamekuja na kitu kinachoitwa easy loan yaani mkopo rahisi. Walikuwa wakitembelea sehemu mbali za Tanzania.

Mimi ni muhanga wa hii benki niliingia nao mkataba wa mkopo wa milioni 1 zimeshapita wiki tatu hadi leo hizo pesa sijazipata. Mimi nipo wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma.

Kama kuna wahanga wenzangu kama mimi ndani ya wilaya ya Kasulu na Buhigwe kwa uzi huu tupeane contact ili tuwe kitu kimoja tufike pale kwenye osifi zao za Kasulu watufafanulie na ikiwezekana hata kuvunja mikataba na benki hiyo tuvunje.
 
Vp jamani me nina mwezi na wiki moja sijapata nishaurini jamani
 
Angalia ndani kama unazo qualification za kupewa mkopo:-

BancABC

TAHADHARI: Website yao imejaa virusi.
 
Walikwambia itachukua muda gani? Umejaribu kuwapigia wamesemaje?
 
Sasa wewe jamaa hiyo bank ipo wapi kwa kasulu? maana kasulu kuna bank mbili tu NMB na CRDB, mnakopa kopa tu hata sehemu zisizoeleweka au ndo umetokea kagera nkanda nini daaah.....
 
ni matapeli. kuna mwalimu anahangaika hadi leo na hatma yake haijui. alikopa m5 wanataka alipe m 13
 
Dah!.. mimi mwenywe ni muhanga, ni wiki ya tatu tangu nijaze mkataba nao na wanadai eti mwajiri wangu ndio hajasign. Hawa jamaa nahisi kuna tatizo wanalo sio kasulu tu maana mimi sipo huko.
 
Jamani angalieni sana kuhusu hii mikopo, tusiingie kichwa kichwa kila tusikiapo mkopo! Ni vizuri kuitathmini sana hiyo mikopo na banki ikopeshayo, vinginevyo ndiyo haya. Halafu kama hujapewa mkopo jaribu kuwafuatilia na kuwaulizia ulizia kwani si contact unazo!?
 
nikadhani BANC ABC hao jamaa nitawalaani maisha yangu yote walichonifanyia sitaki hata kukumbuka.
 
Nchi Hii Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Anapambana Na Betting Huku Banks Kama Kawaida
 
Ishu sio bank ABC, benki zote zote huu usumbufu unaweza kutana nao.

Nilishaenda benki ya posta nilikaa mwezi na wiki kadhaa hadi shida iliyonipelekea kuchukua mkopo nikawa nimeitatua na nikaenda kusitisha huo mkopo wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…