Kuhusu ACT - Wazalendo kuunga mkono Serikali, acha leo niteme nyongo

Kama umeshamaliza kutema hiyo nyongo, wahi sasa ukapige mswaki, oga, kula chakula cha mchana! Halafu nenda ukapumzishe akili.

Baadaye usisahau kuangalia mechi ya Polisi Tanzania dhidi ya Wananchi Yanga.
 
Ukiwa kwenye serekali ndio huwezi kuipinga? Ruto ni makamu wa rais hapo Kenya na anampinga rais wake wazi wazi. Hilo moja.

Aina ya siasa afanyazo Zito kama atapata uungwaji mkono wa wapinzani huku bara basi ni kidogo mno, ama apate support fulani ya wanaccm wasiokubali kushindwa na kuona fedheha ya kushidwa na cdm. Mfano mrahisi toka amefariki Magufuli ACT wameshiriki chaguzi zote za marudio, ukiacha kura chache walizopata kwenye chaguzi za huku bara,bado hamasa iliyokuwepo ya wapiga kura ilikuwa ndogo sana, kwani wananchi wameona ni ccm na mshirika wake ndio wako kwenye huo uchaguzi.

Cdm imefanikiwa kujenga wafuasi wake kuwa na imani kwake, hakuna uwezekano tena wa kuwabadilisha hata kama cdm ikifutwa, sana sana wafuasi wake ambao ni maelfu kwa maelfu hawatapiga kura,na hilo litapelekea chaguzi kuendelea kudoda.

Ukiwa kwenye serekali ndio huwezi kuipinga? Ruto ni makamu wa rais hapo Kenya na anampinga rais wake wazi wazi. Hilo moja.

Aina ya siasa afanyazo Zito kama atapata uungwaji mkono wa wapinzani huku bara basi ni kidogo mno, ama apate support fulani ya wanaccm wasiokubali kushindwa na kuona fedheha ya kushidwa na cdm. Mfano mrahisi toka amefariki Magufuli ACT wameshiriki chaguzi zote za marudio, ukiacha kura chache walizopata kwenye chaguzi za huku bara,bado hamasa iliyokuwepo ya wapiga kura ilikuwa ndogo sana, kwani wananchi wameona ni ccm na mshirika wake ndio wako kwenye huo uchaguzi. Huko Zanzibar hasa Pemba ndiko ACT ilipo na nguvu,na sio kwa sababu ya siasa za ACT, bali kivuli cha Maalim Seif na uadui wa jadi wa watu wa huko dhidi ya ccm.

Katika kitu cdm wamefanikiwa huku bara ni kujenga imani kwa wafuasi wake ambao huwabadikishi kirahisi. Cdm ina baa ya uhakika ya wapiga kura huku bara ambao sio rahisi ccm au Zito na chama chake kuwapata hata cdm ikifutwa. Mfano mrahisi wakati wa uchaguzi mkuu, Magufuli na ccm wakijiaminisha wamemaliza cdm, walichokiona kwenye kampeni, na matokeo yaliyokuwa kwenye box la kura, ukiachia wapiga kura wachache waliojitokeza, ilikuwa ni aibu na fedheha kwa ccm. Nadhani uliona afya ya Magufuli ilivyopata mgogoro wakati wa kampeni, na msongo wa mawazo aliopata baada ya matokeo. Hadi anafariki Magufuli hakuwahi kurudi kuwa normal. Hao cdm mnaojiaminisha kuwa wamekufa, wakirudi tena kwenye siasa za majukwaani ni dakika tu kuwavuga CCM. Hapo ndio utaona tena vyombo vya dola vikiagizwa kuibeba CCM.
 
Ndio siyo sawa kupinga kila kitu na sidhani kama Chadema wanapinga kila kitu siyo kweli. Serikali inahamasisha watu kuchanjwa dhidi ya ugonjwa wa uviko19, Chadema wameunga mkono, tunamuona Sugu akihamasisha watu kuchanjwa.
Unashauri Tundu Lisu arudi afanyie siasa hapa,ni sawa uwepo wake hapa utakuwa na impact kubwa, lakini siyo kupuuza hofu ya kiusalama dhidi ya waliotaka kumuua mchana kweupe, mpaka leo bado yupo IGP yuleyule aliyekuwepo wakati anashambuliwa, na hakuna aliyekamatwa mpaka Sasa.Unawekaje rehani maisha yako kwa walinda usalama wa design hiyo! Hasara ya kupoteza maisha siyo sifa ya maana kwa kujiweka kwenye mazingira ya hatarishi kijinga.
Huyo Maalim Seif kapitia madhira gani yaliyotishia maisha yake? Hii kukamatwa kamatwa mbona Chadema karibu viongozi wote ndo yamekuwa maisha yao.
Chadema kuwakasirikia ACT wako sahihi kabisa,Zito anafahamika vizuri tu, kwani akiunga mkono serikali bila kusema angepungukiwa Nini?
Wenzake, mwenyekiti wao kakamatwa na kuwekwa jela kwa kesi tata,hata Zito mwenyewe anajua,halafu huyo huyo anayemwonea kiongozi wao wewe utangaze kushirikiana naye!! ACT kuwamo ndani ya serikali hakuwajengi kokote,ilianza Cuf kuingia serikalini wamefika wapi? CCM wanajua hawakubaliki popote,wanawaibia kura halafu wanawadanganyia serikali ya umoja wa kitaifa. Kwanza mara nyingi serikali za hivi huwa ni za mpito wakati mnarekebisha kasoro zilizosababisha kuwepo kwa mfumo huo wa serikali.Angalia Kenya baada ya machafuko ya 2007, waliunda serikali ya hivyo, huku waliitengeneza katiba ya kuondoa kasoro za uchaguzi, ndio sababu pamoja na NASA kuwa na wabunge wengi kwa sehemu kubwa bado haikuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Achana na kitu kinachoitwa masilahi (pesa),msishangae.
 
Hakuna muafaka hapo, kuna kujipendekeza tu.
 
Umenikumbusha miaka ya 1980s Denis Healy wa chama cha Labour Uingereza aliposimama Bungeni na kusema kwa mara ya kwanza amewagundua Wabunge wa Conservative wamesema ukweli Bungeni bila kukusudia!! (kwa maana kuwa si kawaida yao!!)
 
Amen, amen
 
Zito Kabwe anafikiria pesa, hafikirii Wazanzibar wengi waliopoteza maisha yao kuitafuta haki ambayo mpaka leo haijapatikana.

Zitto anatumia damu za Wazanzibari kuyafikia malengo yake binafsi ya cheo na pesa. Hajawahi kwenda kuwaaambia Wazanzibari ambao wamekuwa wakipoteza ndugu zao, wamekuwa wakipata vilema, wamekuwa wakiporwa ushindi wao, ni kwa namna gani muafaka wa sasa umehitimisha hayo.

Mwaka 2025 Wazanzibari watakufa tena, wataporwa ushindi tena, halafu Zitto ataenda kwenye muafaka tena ili kujihakikishia mapato binafsi.
 
CDM kama chama wametoa statement ya kuwaponda ACT? au ni baadhi ya wanachama wa CDM ndio wametoa maoni yao.
 
Mimi naona Chadema wako sahihi na Act-Wazalendo wako sahihi pia - maana haiwezekani Chadema waseme au watende kile Act-Wazalendo watakachosema au kitenda na vice-versa.
 
CHADEMA ni kama unavyoona tu Taliban,Alkaida,LRA, M23, Boko Haramu, Alkaida,M4C n.k. ni vikundi mkakati vya kuharibu amani ya dunia kwa upande wa Afrika. CHADEMA wamejificha kupitia mwamvuli wa Siasa ila ukisikiliza sauti zao ni Magaidi,Matapeli na Wachochezi. Sifa kubwa ya makundi haya ni viongozi wao kuishi kwenye makasino ulaya mfano Lisu,Lema,Roma etc. Pia sifa yao nyingine kubwa ni kuwa hawana ofisi maalumu inayoweza kwenda ukawapata viongozi wake. Mara leo Sudan,mara wapo Congo,mara Kenya na sasa wanawasha moto Msumbiji. Sifa ya tatu viongozi wao kusakwa na kushikiliwa na vyombo vya dola mfano Msumbiji Ally na Tanzania Mbowe.
 
Cdm imefanikiwa kujenga wafuasi wake kuwa na imani kwake, hakuna uwezekano tena wa kuwabadilisha hata kama cdm ikfutwa, sana sana wafuasi wake ambao ni maelfu kwa maelfu hawatapiga kura,
Kumbe lengo ni cdm tu na si upinzani?
Hao wafuasi nao chenga basi
 
Mkumbushe. Kasahau huyo. "Birds (ACT and CCM) of the same feather fly together".
 
ACT Wazalendo ni moawapo ya vyama vya upinzani bara kama ilivyo Chadema. Kwa sababu hiyo vyama hivi vina haki ya kujipangia mambo yake yenyewe bila kuingiliwa na kingine. Kukosolewa sio kuingiliwa. Chadema wana haki kuikosoa na kutofautiana na ACT na vyama vingine kama vile ACT walivyokuwa na haki ya kukosoa na kutofautiana na Chadema na vyama vingine. ACT kwa kubali kuwa sehemu ya serikali ya Zanzibar ni lazima wakubali kuwa mapungufu na mafanikio yote ya serikali hiyo ni yao pia. Zanzibar,ACT sio wapinzani wa serikali bali ni sehemu ya hiyo serikali. Kwa vile wao na CCM ndio wanaunda hiyo serikali wasilalamike kama wenzao watashindwa kuona tofauti kati yao na CCM kisiwani huko. Ukitangaza wazi kuunga mkono serikali huku bara ni kuwa unakuwa karibu zaidi na TLP kuliko NCCR Mageuzi. Ni haki yao kufanya hivyo lakini wakubali pia repercussion zake.

Amandla...
 
Kwani ukiwa mpinzani ni kupinga kila kitu?
Sasa unaanzaje kujiita mpinzani tu bila kueleza unapinga nini? Kwahiyo hapo lazima upinge tu kila kitu maana ndio maana halisi ya jina mpinzani ina maana ni mwnye kupinga tu hadi pale utakapofanikiwa kushika madaraka wewe ndipo upinzani utakoma.
 
Lini Chadema walijifunza siasa kutoka Zanzibar? Unasema chama ambacho vongozi na wafuasi wake wako ndani kwa kufanya siasa, ambacho kila siku kiko mtaani kushinikiza Katiba Mpya ndio kinataka kipewe nchi kwenye kisahani cha chai wakati kile ambacho hakifanyi juhudi yoyote kudai katiba mpya, ambacho kinabembeleza serikali iwape haki zake za kufanya siasa unakiona kuwa revolutionary!
Ndio maana unamuita Zitto ginious,

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…