Kuhusu AZAMTV: Je Huu Ni UNAZI wa Mchambuzi, KULIALIA Kwa Yanga au Hujuma?

PROSPER 05

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
226
Reaction score
217
Kuna taarifa imekuwa ikipita ktk Mitandao hasa Whtsapp ikimnukuu Dr LIAKEY. akiwashutumu AZAMTV kuihujumu YANGA na kuibeba Simba. Je ina ukweli wowote.
SOMA MADAI YAKE HAPA CHINI
" Mchambuzi wa soka mwenye uzoefu mkubwa nchini DR.LIAKEY ABDALAH amemponda mrusha matangazo wa azam TV kwamba anakuza matukio na kuchelewesha camera kitu ambacho kinachonganisha marefarii na washka vbendera kwa bodi ya ligi. Amesema ameangalia mabao ya Simba na ya Yanga amegundua kila mchezaji wa Yanga anapofunga goal Mpiga picha wa Azam ana scroll camera aoneshe kaotea. Kasema maelezo hayo ameyatoa kwa mpiga picha ambaye ni rafiki yake anaerusha ligi kuu ya uingereza kuptia TV1. Amedai kuna kitu kinachofanywa na Azam Tv kuupotosha umma."

NI KWELI KUNA HUJUMA?
 
hata siajelewa..... kama kuna mtu amemsoma huyu mdau aniambie
 
nini teena hii?mi huwa nakuwepo uwanjani kwa hyo hoja kuwa offside za simba na yanga hasa zinapocheza na timu zingne marefarii wanapotezea!!!!!YANGA NDIO TIMU AMBAYO INAONGOZA KWA KUBEBWA NA MAREFARII!!!!!
 
Huyu mwandishi kaandika kisukuma?

Kiswahili lugha ya taifa hawezi sasa kisukuma labda tumwelewe atuandikie hapa
 
Hakuna editing ya haraka kiasi hich😵ffside za yanga huonekana wazi hata kwa walio uwanjani.Marefa wetu ni wabovu tu,acheni utetezi usio na mashaka.
 
Huyo Anaijiita Dr liki anazeeka vibaya.... Habari za uchambuzi zishampita.
 
Reactions: PNC
Kitu ni simple na dhahiri. Azam wanachezea teknologia ili ionekane Yanga inapendelewa na waamuzi.
Watu walishaliona hilo toka mwanzo. Azam mmiliki watimu mmojawapo na mmiliki wa Tv.
Hatuna Sky Sports wa kuwa neutral hapa kwetu.
Azam huyo huyo ndiyo mdhamini wa ligi kupitia Tv yake.
Nani asiyejua Azam alikuwa Simba kabla ya kuanzisha timu yake?
Madai ya Dr. Leakey yasipuuzwe. Hii teknologia ni mpya Tanzania. Wengi hatujui undani wake.
Azam Tv wanafanya mno analysis ya magoli ya Yanga kuliko hata ya timu yao mbovu licha ya kuwekeza mabillion!
Wachambuzi kwenye Azam Tv wanatetea maslahi ya boss anayewalipa
Ubovu wa timu yao wanaongelea juu juu sana. Ingekuwa ni Yanga tusingekunywa maji mjini!
 
Goli la pili la Mbeya City kama ingelikuwa la Yanga, Azam wangerudia mara mia kuonyesha halikuwa halali. Lakini kwa kuwa kafungwa Yanga, roho zao kwatu. Wachambuzi "wao" wataufyata tu. Na yule mwamuzi aliyefungiwa kwa rushwa ya dhahiri lakini akaja kusamehewa kimuujiza angeimba kama kasuku.
 
Ukweli azam tv ni kero kubwa na kama mnaendeleza huu unazi wenu biashara itawashinda
 
mmepigwa na stand united... mmepigwa na mbeya city.... halafu mnaleta kuhujumiwa hapa
 
Reactions: PNC
Hakuna editing ya haraka kiasi hich😵ffside za yanga huonekana wazi hata kwa walio uwanjani.Marefa wetu ni wabovu tu,acheni utetezi usio na mashaka.
ikitokea offside kwa yanga azam wako fasta kutoa rekodi,jana yanga kafungwa goli la utata azam kimya mpaka sasa unaliongeleaje hili mwalimu kashasha.
 
Kwanini usianzishe TV station na uchukue haki miliki ya kuonyesha Mpira Wa ligi kuu Tanzania bara aubumwambie manji afanye hivyo... kama hoja no azam alikuwa simba, he Jamal Malinzi alishaacha uanachama yanga? tuache upumbavu na unazibwa kisengerema...nyeusi nyeusi kamwe tusiilazimishe kuwa nyeupe
 
Mse
Msengerema atukuwa baba yako. Unadhani kila mtu yupo huko. Hijo de puta.
Huwezi kujenga hoja bila kumtukana mtu? Somebody crashed on your madre and damaged your brain.
 
Yanga ingekua inaongoza ligi haya yote yasingesikika.

Halafu mtu kama Liki anajua soka, hv ni kweli mtu hakua offside then, uscroll kamera anakua offside? NONESENSE kabisa hii.
Aisee..........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…