Yaani hapo jibu rahisi ni wewe utaingia gharama ya kupaka rangi na kuweka engine mounting mpya..Nilipata ajali na gari ikakaguliwa na vehicle inspector na akaandika report baada ya kuipeleka gereji, malipo yameandaliwa na mwenye gereji akakubali kutengeneza kutokana na malipo yaliyokubaliwa lkn wakati kazi inaendelea ikagundulika kuwa kuna tatizo "engine mounting" nayo imekatika na gari inatakiwa kupakwa rangi upya, nafanyaje?
i. Ninaweza kuwaandikia ili niongezewe kiasi kinachoongezeka?
i. Inatakiwa nitengeneze kwa gharama zangu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kuna ishu ta Utmost good faith lakini pia kwenye bima wana-assume kwamba mteja yeyote anachukuliwa hajui masuala ya bima hivyo ni muhimu kuelekezwa.Kweny bima kuna kitu kinaitwa Principle of utmost good faith
Yani ww unatakiwa useme ukwel wa kila kitu kuhusu gari lako...sasa hapo kweny gharama,una expose gharama mpya tofaut na mwanzo utaonekana una breach hyo principle..yan watahis unaleta janja janja..so jichange tu umalze hilo tatizo lako
Sent from my SM-G920P using Tapatalk
Sure..nilivyosema amevunja sikumaanisha direct ni yeye ..Ni kweli kuna ishu ta Utmost good faith lakini pia kwenye bima wana-assume kwamba mteja yeyote anachukuliwa hajui masuala ya bima hivyo ni muhimu kuelekezwa.
Pili hajavunja Principle ya utmost good faith kwa sababu si yeye aliyeandaa repair estimate na pia yeye si mtaalam wa magari, pale ambapo bima na repairer walikubaliana kutengeneza mteja jukumu lake ni kuhakikisha analikuta gari lipo katika hali iliyokuwapo kabla ya ajali.
Suluhisho ni kwa mteja kumwambia repairer awaandikie bima juu ya tatizo lililoongezeka na gharama zake. Maadam tatizo hilo limetokana na ajali iliyotokea. Halafu garage huwa wanapewa pia miscellenaous additional cost nayo bima wataangalia ili kupunguza gharama!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sure..nilivyosema amevunja sikumaanisha direct ni yeye ..
Ajarbu hiyo suggestion yako..ila hawa jamaa hawakawii kusema kala njama na fundi
Sent from my SM-G920P using Tapatalk
Yes, hayo mazingira yanakuwa so suspicious. Maana rangi ilitakiwa kuonekana mapema.Hadi swala la kupaka rangi halikuonekana mapema?
Engine mounting inaweza kuwa technical, ila swala la rangi sijaelewa kwa nini halikuonekana mapema.