MenukaJr
Member
- Apr 24, 2021
- 50
- 128
Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali iliyotolewa tarehe 05 June, 2021 imebainisha kwamba Rais wa JMT amepokea tayari taarifa mbili kutoka katika Kamati aliyoiunda kwa ajili ya kufuatilia na kuishauri Serikali namna ya kupambana na gonjwa la corona. Taarifa ya kwanza ilikua ni yenye maoni ya namna Serikali inavyoweza kupambana na corona na taarifa ya pili inahusu namna ambavyo Serikali inaweza kupata rasilimali (nadhani fedha) kwa ajili ya kupambana na corona.
Kwa mantiki ya kawaida, taarifa ya pili ya Kamati imeamua tayari msimamo wa Serikali juu ya corona. Kwa kawaida huwezi kufikiria kutafuta fedha kwa jambo ambalo bado kulifanyia uamuzi. Kwa hiyo, taarifa ya kwamba Baraza la Mawaziri litaketi hivi karibuni kuamua iwapo Serikali ikubaliane na chanjo au la ni ya uongo (danganya toto). Ukweli Serikali itakua tayari imeamua kuruhusu chanjo ndio maana imeagiza Kamati kupendekeza namna ya kupata fedha kwa ajili ya kununulia na kusambaza chanjo. Ndiyo maana pia imeruhusu Watanzania wenye kufanya kazi katika mashirika na taasisi za nje hapa nchini kuchanjwa.
Kwa sababu hiyo, kama Mwananchi mwenye HAKI ya kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba, kama raia mwenye kuhusika na chanjo hiyo moja kwa moja, kwa ajili ya kumbukumbu natoa maoni yangu binafsi kwa Serikali kuelekea kikao cha Baraza la Mawaziri la uamuzi.
1. Kabla ya kuamua kutangaza kuleta chanjo Serikali itambue kuwa chanjo ya corona haizuii maambukizi ya corona wala haiondoi masharti ya kujikinga na corona kwa uzoefu wa taarifa zilizopo. Taarifa zinasema mwenye kuchanjwa anaweza kuambukizwa sawa na asiyechanjwa. Tutafakari umhimu wake kulinganisha na madhara ya corona katika nchi yetu tusije kurudi nyuma.
2. Kabla ya kuamua kutangaza kuleta chanjo, Serikali itambue kuwa chanjo ya corona ni biashara ya Mataifa yenye nguvu. Kwa vyovyote ili tuhimili gharama za chanjo itatupasa kukopa pesa zaidi kwao pamoja na mashirika ya fedha Duniani. Hadi sasa nchi yetu inadaiwa zaidi ya Tshs. 60 trioni. Hiki ni kiasi cha juu ukilinganisha na mahitaji ya pesa yaliyopo ili kugharamia miradi ya maendeleo. Kama hatukuwa makini, tunaweza kukopa pesa nyingi kwa ajili ya corona na kulifanya deni letu kuwa kubwa zaidi lisilohimilika au kushindwa kukamilisha miradi yetu ya maendeleo, tutarudi nyuma.
3. Kabla ya kuamua kutangaza kuleta chanjo, Serikali itambue kuwa nchi yetu haina uwezo wa kuchanja hata theluthi moja ya watu wake kwa miaka mingi zaidi. Mathalani, tangu February mwaka huu nchi ya Afrika Kusini imechanja watu 481k tu sawa na wastani wa watu 160k kwa mwezi. Kwa takwimu hii, itawahitaji miaka 30 kuwachanja watu wake wote. Idadi ya Wa-South Africa haitofautiani sana na sisi. Swali la kujiuliza, tunawezaje kuchukua jitihada za kukinga watu wetu ili tuikamilishe miaka 30 ijayo. Kati ya sasa na wakati huo tutakua tumepoteza watu wangapi (kama kweli tatizo lipo), tutakua tumepoteza pesa kiasi gani. Kwa vyovyote vile njia hii haiwezi kuwa na maana yoyote zaidi ya upotevu wa pesa.
4. Kabla ya kutangaza kuleta chanjo, Serikali yetu itambue kuwa kwa sasa corona sio tishio tena Duniani na kwa sababu hiyo isifanye uamuzi under a such serious tension. Tunaweza kulichukua jambo hili kwa taratibu wakati namna bora na rahisi zaidi zikiendelea kuvumbuliwa. Nchi nyingi (kama sio zote) zimefungulia watu wake kuendelea na shughuli zao kama kawaida, zimeanza kuipuuza corona. Nimeangalia fainali za Kombe la Ulaya (UEFA) mashabiki wameruhusiwa kuingia uwanjani, hata sasa mechi za kirafiki za FIFA mashabiki wanaingia uwanjani wengine wamevaa barakoa wengine hawakuvaa, hii ina maana moja tu kubwa; tunaweza kuishi na corona. Hatua hii sisi tuliipita muda mrefu na JPM hatupaswi kurudi nyuma na Samia Suluhu.
5. Kabla ya kutangaza kuleta chanjo, Serikali itambue endapo ni lazima iruhusu chanjo kufuata Itifaki ya Dunia inaweza kutumia njia mbili; MOSI. Iombe kupata chanjo za corona bila gharama (free of charge). PILI. Iruhusu wenye kutaka kuchanja (kwa ajili ya safari nk.) watafute chanjo kokote wachanje nje ya gharama za Serikali ikiwa ni lazima kufanya hivyo. Kusudi la njia hizi ni kuiondoa Serikali katika gharama zisizo na lazima.
HITIMISHO. Dunia inacheza kamari katika tatizo hili la corona. Kwa kawaida kwenye kamari wajinga ndio wenye kuliwa nyingi.Tanzania tumepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya corona, tumelipa gharama yake kuliko nchi yoyote katika Dunia hii kwa vyovyote hatupaswi kulipa gharama kwa mara nyingine tena kwa ajili ya chanjo. Watanzania badala ya ku-sign petition ili Diamond asishinde BET tunaweza ku-sign petition kupinga matumizi ya fedha zetu kwa ajili ya chanjo, inaweza kutuheshimisha!
#TutakukumbukaDaimaJPM.
MenukaJr,
Da'slama-Tanzania.