Kuhusu CV na PhD ya Dr. Slaa

Status
Not open for further replies.
Afadhali tuachie hapo na tusichokoze zaidi halafu watu wakaanza kusema hovyo wakati wengine tunawaheshimu sana.
 
Hebu msitake kuchakachua elimu hapa...mtasema kuwa hicho chuo kina affiliation na university fulani ila tembea dunia yote hii katafute chuo kinachotoa Phd kwa mtu mwenye diploma...
mfumo ni huu...unasoma bachelor..masters..then Phd.
Ni wapuuzi tu watakaoshabikia uchakachuaji wa elimu kama huu.
leteni mfumo huo hapa Tz basi ili tuache kuhangaika na degree,na masters.napiga zangu diploma ya ualimu then nafanya Phd.
 
Mwaka 1958 alikuwa darasa la kwanza. Mwaka huu ana mtoto mchanga! Mzee wetu huyu naye?!
 
mi nafikiri point si mtu ana PHD au laa, tumeshaona watu wengi sana PHD's ila mibichwa kama madafu na mifano hai tunayo LIVE. Mwacheni DR. wetu wa ukweli na nyie si mnae sasa mbona mnatufuata fuata?

Magamba yameshindwa kukoboka mnaanza kuleta hoja zisizo ma mashiko, Wekeni GPA ya DR. wenu tuione alipomaliza Bsc yake.
 

Hapa mkuu umekosea!
Prof Lipumba ni one of the best professors wa Economics. Ni world renown consultant kwenye maswala yanayohusu economics, he does a lot for world bank na IMF. Kati ya wanasiasa wote nchini, yeye ndio mwenye CV iliyoenda shule. Pamoja na Dr Slaa kuwa better politician, he is no where close to Prof Lipumba kwenye maswala ya Academics, no where!!
 
safi sana FJM umenielewesha vizuri sana mambo mengi sikua nayajua...
 
<br />
<br />
Nakubaliana na wewe kuhusu kisomo cha prof. Lipumba ila kitu ambacho nataka unielewe ni kuwa kipindi hiki si cha kuangalia elimu kiasi gani mtu anayo bali nikindi cha kujiuliza je elimu niliyo nayo inasaidiaje maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla. Si prof. Lipumba tu bali wako wengi umeona kama Dr. Kafumu anajisifu kuhusu CV yake akiwa kama mtaalam wa madini katika wizara ya nishati na madini lakini ni hao hao ambao wametuingiza kwenye mikataba mibovu ya umeme na migodi. Kwa ujumla nadhani kuwa na sifa nyingi ni zake binafsi kielimu ila tukija kwenye upande wa maendeleo ya taifa mchango wake unaweza kuwa mdogo sana. Ndio maana bado nasema kwa elimu ya Dr. Slaa haina ya kuhoji sana kwani shule aliyo nayo inatosha kuwa kiongozi wetu na mchango wake kwa taifa huna haja ya kuhoji na mpaka mtoto wa darasa la tatu vijijini anajua mchango wake.

Nawakilisha
 

Awali ya yote napenda kukufahamisha mimi sio Mhasibu bali ni mchumi kuanzia Bcom (Udsm-Tz) MBA (Ontario- Can) na PhD (Sofia- JPN). Sijawahi kuwa Mhasibu popote pale katika maisha yangu zaidi kufanya kazi Wizara ya Mipango na baadae kuwa RDD(Regional Development Director- Mwanza. Kabla kurudi Nyumbani Oman (kuukana uraia wa Tz na kuchukua uraia wa Oman).

ndugu yangu Sikonge,
Si kuwa naipenda CCM au chama chochote huko Tz bali nazungumzia hali halisi enu ya Uchumi kama field yangu kwani naguswa sana na maisha ya jamaa, marafiki na hata ndugu zngu huko wanavyoishi na namna nchi inavyoendeshwa.

Kama kawaida yangu kwangu kuimarisha uchumi ni jambo la kwanza na mengine kama siasa ni baadae nacho ni kitu kilichonifanya niondoke TZ. Lakini napenda kukujuza Biashara zangu zoooote ni clean kabisa tunafata sheria zote za nchi yenu na hata ukitaka waambie TRA wakaangalie na kama una ushahidi wowote basi peleka kwenye vyombo husika ili hakhi itendeke. Tupo wazi kwa hilo. Na Mke wangu yapo kama mwanasheria basi mkaonane mahakamani.

Lakini kama mwanadamu ulie sahihi kabisa unatakiwa uhoji kila kitu. Haingii akilini mchumi kama mimi unaniweka kwenye mambo ya medicine ni lazima ujiulize mara mbili.

Nikirudi kwa Dr Slaa , kila wakti namuuliza kwa elimu yako hiyo Je madhehebu mengine huko TZ au waislam watakuwa salama kama wewe ukipewa nchi? Ni nani asiyejua kanisa katoliki na Mtandao wake kuanzia jumuiya zake za Mitaa, kigango, parokia mpaka Taifa.

Je angekuwa Mtu amesomea Uislam kama Prof Juma Mikidadi (aliyewahi kuwa Mbunge wa Kibiti- Rufiji ) ambaye alisomea Islamic Law mpaka masters ake na kisha PhD. Je wakatoliki wangekuwa kimya.

Lakini yote hayo yanataka mtu makini katika kuhoji na hata kujua ukweli wa mambo na kujiridhisha kwa nia ile ile ya mustakabali mzuri wa ustawi wa nchi yako.

Usione Khaya kuhoji kwani ndiko kunakokupa mwangaza wa baadae. Usipende kitu kiasi cha kuona kwenye chongo ukasema kengeza.

By The way, ndugu zangu huko Sikonge wazima? nasikia kuna njaa sana na inshallah nitapeleka chochote soon kuwasaidia.
 

Nilipo Blue,
Je unajuwa CAN LAW?
 
basi phd anayo nan ni aibu kuona watu kama nyie kwenye hii safu unadhani mtu anayetoa mawazo ana uwezo wakutoa wazo zuri kumbe hamna kitu unashindwa kujua hata profile ya mtu mahil mim nna uhakika hata profile ya kikwete hujui niambie hatua kwa hatua phd
 
Mwacheni Dr Silaa bhana yupo juu kielimu katika dunia hii sio presidaa wenu ambaye elimu yake inafanana ya mbunge Lema, amekalia kupewa suti na waarabu ili asafirishe wanyamapori.
 
Kuna watu wengine mlisoma lkn elimu zenu hazina maana kwa nchi yenu, ulifikia hadi cheo ya RDD lkn udini haukukutoka. Hebu fikiria kama waislamu ndio wangejenga shule wakati wa ukoloni si nchi nzima mngewalazimisha wawe waislamu. Samahani sana baba yangu lkn uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana na elimu yako hiyo ya kujifungia na madesa kwenye msikiti wa udsm ndio iliyokuharibu huko nyuma.
 
Sawa kabisa kaka, kama mtu akitaka kuelewa kitu afanye utafiti kwanza kabla ya kuongea. Na utafiti unaweza kufanyika kwa kumhoji Dr. Slaa. Na swala jingine ni kwamba Chuo kilichompa Dr Slaa hiyo PhD kipo na amekitaja sasa kwa nini asiulize huko anatafuta majibu sehemu nyingine?
 

Huo ndio wasi wasi wangu si kwa Dr Slaa lakini pekee lakini pia hata kwa Chadema. Kwani kimejengwa katika misingi ya Kikanda (Ukaskazini) na Ukristo. Lakini pia Elimu ya Mtendaji mkuu na maisha yake akiwa mseja na nikilinganisha na niliojifunza tanganyika na kuyaona UDINI unavyo tawala japo umefunikwa na joho zuri sana na mawazo ya wakristo wengi huko dhidi a waislam naona kuna mustakhabali mbaya tena sana..

Napata mashaka na maendeleo ya nchi yenu. Nafikiri ni wakti wenu kujitathmini na kuangalia mustakabhali wa nchi yenu yasije tokea yale ya Suudan,

nawapa pole.
 

hatufanyi utafiti kwa kumuuliza tu lakini hata kuangalia makuzi yake ya utotoni na ujana wake pia kuangalia elimu yake na mtiririko mzima wa maisha yake .

hayo yanaweza kabisa kukupa mwanga wa kuweza kumtambua mtu. Japo watu huwa wa badilika lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.
 
Naamini tutakuwa tunapoteza muelekeo kudhani kuwa PhD au Masters nk ndizo zinazomuwezesha mhusika kuwa na mchango wenye tija katika jamii. Elimu mtu anayoipata inakuwa na manufaa pale inapoelekezwa kwenye mchango wenye tija kwa jamii husika, kinyume cha hapo inabakia kuwa sawasawa na maiti iliyosheheni nguo, manukato na vidani vya thamani wakati kwa ndani imeharibika na vikolombwezo hivyo haviongezi tija yeyote.
Kwa wenye kumbukumbu nzuri mwanzoni mwa miaka ya 90 aliteuliwa waziri mmoja msomi Profesa wa uchumi kuongoza wizara ya fedha, katika kipindi chake aliivuruga uchumi wa Tanzania na mfumuko wa bei kufikia asilimia 30% na aliendelea hivyo hadi nchi wafadhili wakatishia kusimamisha misaada baada ya nchi kuwa taabani kabisa. Kilichotokea alilazimishwa kujiuzulu na ndipo akateuliwa Raisi aliyeko madarakani sasa kuongoza wizara hiyo.
 

Kama kweli una PhD kama usemavyo, basi elimu yako uliipata madrasa, siamini kama kweli Mchumi anaweza kuandika vitu kama ulivyoandika hapa! Afadhali ya mtu mwenye pass kama Kikwete kuliko wewe!
 
Nilipo Blue,
Je unajuwa CAN LAW?

Katika threadi hii nimeuliza maswali manne ambayo niliyaelekeza kwako na wachangiaji wengine ili tupate uelewa wa kinagaubaga kuhusu PhD ya Dr. Slaa. Naomba ujibu hayo maswali. Ukijibu yote kwa pamoja itakuwa vizuri sana. Kama unaona ni mengi kuyajibu kwa wakati mmoja, naomba ujibu mawaili ya kwanza yaani 1. na 2. Halafu umalizie 3. na 4 baadaye. Nami nitajitahidi kutafuta majibu ya swali lako na kukujibu baada ya kupata kutoka kwako majibu ya maswali yangu, angalau mawili ya mwanzo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…