Walibadilisha sheria ya makato kutoka 8% mpaka 15%. Mabadiliko haya yakawahusu hadi wale ambao walikuwa wanakatwa 8% katika mshahara. Wadau walipiga kelele lakini bodi hawakujali.
Sasa wameanza tena uhabaishaji wao kwa kuongeza makato (retention fee) kitu ambacho hakipo katika mikataba ambayo tulisaini miaka hiyo mfano mkataba wa bodi wa mwaka 2009.
Bodi wanatakiwa waheshimu mikataba tuliyosainishana, mfano mkataba wao wa mwaka 2009.
Bodi wakumbuke kuwa, mabadiliko yoyote hayapaswi kuwaathiri wale ambao tayari wamo katika makubaliano ya awali.
Kukaa kwetu kimya wasidhani tunaridhika na unyanyasaji wao. La hasha! tunasubiri muda tutapata haki yetu na kulipwa fidia kubwaaa.
Ni kwamba, nimeitunza nakala ya mkataba wa bodi niliousaini mwaka 2009.
Pia, kwa sasa, kila mwezi nadownload salary slip, nazi save kwenye mtandao, pia naziprint mpaka nitakapomaliza deni mwaka 2026.Salary slip ikiwa nyeupe, itakuwa ngumu kukubali makato mengine ya bodi, bodi wakilazimisha, itabidi kwenda mahakamani.
Kutokana na kuvunja mkataba, nimepanga kuwashitaki bodi ya mikopo hata kama ni mwaka 2040! Najua ipo siku mahakama itakuwa huru. Kwahiyo, chonde chonde bodi, jaribuni kufikiria future. Mtakuja kulipa fidia kubwa huko mbeleni.
Kwa sasa mmeshika mpini tumekaa kimya ila wengine tuna jambo letu, tunakusanya ushahidi. Cha ajabu, ikifika mwaka 2040 mahakama ikiamua tulipwe pesa ndefu kama fidia, wapo watakaotuona sisi siyo wazalendo, wakati leo tunavunjiwa mikataba, na wamekaa kimyaa.
Ushauri wa bure, bodi iombeni serikali hela ya kuwakopesha wanafunzi, mana ni jukumu la serikali kuwasomesha raia wake. Mnapotaka kujiendesha ndipo mnapoanza kutubambikia madeni, mwisho wa siku tunaishi maisha ya bila furaha.