Kuhusu Kansa ya Damu

Kuhusu Kansa ya Damu

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Wakuu naomba kujua kama huu ugonjwa una tiba au la, kuna ndugu yangu anaumwa hivyo nahitaji kujua tiba yake.
 
Wakuu naomba kujua kama huu ugonjwa una tiba au la, kuna ndugu yangu anaumwa hivyo nahitaji kujua tiba yake.

pole mpendwa me cjui but i lost my grandfather and my school best friend (Always in my mind as she was my 1st best friend).
Waone hawa watakuambia mimi49 MziziMkavu Na madoctor wengine sorry sina id zao kichwani.
 
Last edited by a moderator:
pole mpendwa me cjui but i lost my grandfather and my school best friend (Always in my mind as she was my 1st best friend).
Waone hawa watakuambia mimi49 MziziMkavu Na madoctor wengine sorry sina id zao kichwani.
mkuu pole sana, ok ngoja niwa subili hao ulio wataja hapo MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Leukemia imegawanyika katika makundi manne nayo ni:
  1. Acute myeloid leukemia (AML)
  2. Acute lymphoblastic leukemia (ALL)
  3. Chronic myeloid leukemia (CML)
  4. Chronic lymphocytic leukemia (CLL)
Mtu anapopatwa na ugonjwa huu anakuwa na muongezeko wa kukua/wingi wa chembechembe nyeupe za damu.Leukemiacells zinazuia kutengenezwa kwa chembechembe za kawaida kwenye bonemarrow.Na bonemarrow isipokuwa na uwezo wa kuzalisha chembechembe nyeupe za kutosha mwilini unapatwa na dalili kadhaaa nazo ni:

  • Kudhoofu kwa mwili/hitaji la kutaka kupumzika zaidi
  • Uzito wa pumzi/matatizo kwenye kupumua
  • Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
  • Kizunguzungu
  • Maumivu ya kichwa
  • Homa za maramara na infections za aina tofauti zinazojirudia
  • Kuvia kwa damu mwili,kutoka kwa damu kwenye fizi
  • Kuwa na uvimbe kwenye lymph nodes,ini na spleen
  • Kupungua kwa uzito
  • Kutokwa na wingi wa jasho usiku

Sababu za ugonjwa huu ni:
  • Kurithi haswa kwa wagonjwa wa Chronic Lymphocytic Leukemia
  • Kutibiwa na chemotherapy au mwili kuwa exposed na chemicals au radioactive radiations
  • Wagonjwa wenye chronic myeloid leukemia wana mabadiliko kwenye chromosome mwilini inayoitwa Philadelphiachromosome

Utajuaje kama una kansa ya damu
  • Kipimo cha damu ili kuangalia mabadiliko ya chembechembe za damu mwilini
  • Bonemarrow test
  • Immunophenotype and chromosome test

Tiba za ugonjwa huu:
  • Chemotherapy kwa wiki kadhaa inategemea na kansa ya damu uliyonayo,Kuna aina tofauti za chemotherapy ambazo zinaweza kutumika kama vidonge au intrathecal chemothrapy(Ambapo unatibiwa direct kupitia kwenye spinal cord).
  • Radiation therapy
  • Stam cell transplantation
  • Monochlonal antibodies
  • Kuondolewa kwa spleen
  • Cortison treatment

Wagonjwa wanaopatwa na na Acute myeloid leukemia (AML)/Acute lymphoblastic leukemia (ALL) wana asilimia 80-90 za kupona ugonjwa huu lakini kuna 50% risk ya huu ugonjwa kurudi tena.
Wagonjwa wanaopatwa na Chronic myeloid leukemia (CML)/Chronic lymphocytic leukemia (CLL) hawawezi kupona ugonjwa huu wanaweza kupatiwa tiba ili kupunguza dalili za ugonjwa na kuongeza muda wa kuishi na kawaida wanatabiriwa wana muda gani wa kuishi kutokana na wameathirika kiasi gani!
 
Back
Top Bottom