Kuhusu Kenyata na Ruto: Kweli siasa ni kizungu mkuti

erastosichila

Member
Joined
Jun 8, 2017
Posts
70
Reaction score
42
Tuliaminishwa kuwa Uhuru na Ruto wameshiriki kuua watu uchaguzi mkuu wa Kenya, yakaletwa mashitaka wakapelekwa Thehugue (uholanzi)kesi ikaishia ilipo ishia,kukosa mashahidi.

Hivi Leo hayo hayo ndio wameshinda uchaguzi huu mkuu Odinga anashindwa tena kura 2millioni zaiidi,basi Siasa ni kizungu mkuti ndani ya siasa ni porojo tu afadhali hapa KAZI tu ,wananchi wachape KAZI Siasa ni Ulongo, tu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rekebisha, 1.4.... milioni
 
Hey Lumumba tuliza akili zako uandike vizuri basi!! Hiyo the Hague ndiyo iliyowaunganisha na hatimaye kuunganisha makabila yao (Kikuyu & Kalenjin) kuwa kitu kimoja dhidi ya mtu mwingine yeyote.

Pia ukumbuke Africa bila kuungwa mkono na system (dola) huwezi kupewa nchi hata kama utashinda ki halali kama ilivyotokea Zanzibar 2015.

Cairo's
 

Kesi ya The Hague ilipangwa ili atiwe hatiani asiweze kugombea urais mwaka 2012. Yule jamaa wa Marekani alikuwa anamsaidia ndugu yake ili aweze kuchukua urais. Uhuru hakuwa na hatia tangu mwanzo na hakustahili hata kushtakiwa.

Mpinzani wake ni jamii ya Sivimbi hakubali kushindwa. Katiba yao inaruhusu matokeo kupingwa mahakamani sasa kama ana uhakika alishinda na nakala za fomu za matokeo zenye ushahidi wa pande zote anazo kwa nini asiende mahakamani badala yake wafuasi wake wanatoa maneno ya vitisho, Asiyekubali kushindwa si mashindani. Urais sio suala la zamu bali ni matakwa ya wapiga kura.
 
Mahakama sio suluhisho huwezi kumshitaki rais aliyepo madarakani alafu ukashinda hususani Kenya. Inasemekana jamaa aliyekuwa afisa wa kusimamia uchaguzi alitangulizwa ahera na password yake imetumika kuingiza kura milioni moja za awali yaani fanya ufanyavyo mgombea wao anaongoza kwa kura milioni moja
 

Hizo porojo. Kwani nakala za fomu za vituoni wao NASA hawana? Mahakama ya Kenya ni huru na katiba yao inaruhusu matokeo kupingwa mahakamani
 

Ni Ruto siyo Luto.Mshamba !
 
Hizo porojo. Kwani nakala za fomu za vituoni wao NASA hawana? Mahakama ya Kenya ni huru na katiba yao inaruhusu matokeo kupingwa mahakamani
Unakumbuka Zanzibar 2015 ?! Jibu kama wewe ni mkweli wa nafsi yako [emoji120] Hii ni East Africa bora kidogo West Africa kuna ECOWAS

Cairo's
 
Hii mbona ni kama hadithi ya kwenye vijiwe vya kahawa?Kama unajua hili suala LA mauaji kwanini usiende mahakamani?
 
Mashaidi walianza kuuwawa mpaka wakaogopa kujitokeza kenya ni nchi inayoongozwa na mafia /Cartel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…