Kuhusu kilimo cha bustani kwenye shamba lenye miti mirefu

Yuzoh

New Member
Joined
Nov 6, 2017
Posts
1
Reaction score
0
Wadau habarini za siku! Tuwe pole na majukumu ya kila siku.

Mimi naomba niulize ama mwenye uelewa anijuze;

Nimepanga nyumba fulani ambayo imezungukwa na mipaini au wengine wanaita mibai yaan ile miti ya mbao ila kuna vinafasi vinafai nikaamua kulima bustani ila ukuaji wa miche ya bustani kama vile nyanya, bilingani na bamia sio mzuri hata kidogo yaani upo very slow yaan inadumaa.

Naomba ushauri nifanyeje!
 
Mwanga wa jua ni muhimu sana Kwa mimea, punguzia matawi hiyo miti haraka sana.
 
Ni vyema mboga zioteshwe eneo lenye mwanga wa kutosha ili majani yake yaweze kutengeneza chakula cha mmea. Japo ipo aina ya mimea usiyopenda mwanga mkali wa jua.

Hivyo utajaribu mimea mingi uone ni mimea gani inastawi vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…