Kuhusu kubadilisha tahasusi (Combination)

Kuhusu kubadilisha tahasusi (Combination)

Felice6

New Member
Joined
Jun 2, 2023
Posts
4
Reaction score
1
Habari za muda huu wakuu

Mdogo wangu alimaliza kidato cha nne mwaka jana ambapo ndiyo wamepangwa kidato cha tano. Amepangiwa Combination ya HKL badala ya CBG aliyoitaka na shule alipangiwa zipo combi za sanaa tu, HKL, HGL na HGE. Je, mchakato wa kuhamia shule yenye combine hiyo ukoje?

Msaada
 
Kama shule aliyochaguliwa ina hio kombi anayoitaka hainaga shida hapo itabidi ahame tu!!
 
Kama shule aliyochaguliwa ina hio kombi anayoitaka pia haina shida akaongee na wataaluma tu ila kama haina hio kombi hapo inasumbua kidogo!
Asante, hiyo shule haina hiyo kombi
 
Kwanza mdogo wako ana bahati kuchaguliwa HGL ambayo chuo kikuu unachaguzi kusomea fani nyingi kuliko CBG namshauri asibadilishe . Hii combination ya CBG inawafaa watu wenye ndoto za kuwa waalimu. Ingekuwa alikuwa anahitaji kubadilisha kwenda PCM au PCB hapo sawa. Narudia kama mwambie asome HGL vinginevyo kama ana ndoto za kuwa mwalimu.
 
Back
Top Bottom