Kuhusu kujenga nyumba kwa mkandarasi au fundi wa kawaida...

TGS D

Senior Member
Joined
Aug 3, 2010
Posts
114
Reaction score
13
Habari great thinkers,

Naomba ushauri na maoni yenu kuhusu kujenga nyumba.Kipi ni bora na nafuu iwapo utatumia mkandarasi au fundi wako wa mtaa?

Maoni yenu yatatusaidia wote.
 
Mkuu mkandarasi na TGS D wapi na wapi? au umefisadi mahali?(just kiddin). nadhani ni rahisi ukijenga mwenyewe kwa sisi wadundulizaji
 
Mkuu mkandarasi na TGS D wapi na wapi? au umefisadi mahali?(just kiddin). nadhani ni rahisi ukijenga mwenyewe kwa sisi wadundulizaji

Hahahaaaa,Serikali itakapoapprove 3.5M mkuu
 
Unajua unapompa kazi Mkandarasi ni kwamba tayari amepewa hiyo kandarasi anapata faida kwa hiyo kuna mafundi atawapa hiyo kazi,na watalipwa mshahara na mkandarasi atabaki na faida.Cha msingi we komaa mwenyewe na mafundi wa mtaa.Unaweza tumia 1.5m kutoka msingi hadi renta,lakini ukimpa mkandarasi anaweza taka kwa kazi hiyo tu mpaka renta 10m.Kaa ukijua materials kote mkandarasi au fundi mtaa ni juu yako.
 
Ujenzi hutegemea na mfuko mkuu,kama uko busy na huwezi kufuatilia mafundi na control ya vifaa vya ujenzi ni vizuri kumtumia mkandarasi unaemwamini au anaeaminika akufanyie mtalipana kadili mkataba wenu mtavyoridhiana.

Kama ni pesa za kutafuta kidogo kidogo vema kumtumia fundi wa kawaida.

So inategemea uwezo wako kifedha na aina ya ujenzi coz kwa ujenz wa ghorofa yoyote ni lazima mkandasi auhusishwe na consultants i.e architect na structural eng kwakuwa kama yakitokea madhara hao ndo watajibia bt ikiwa ni wewe mwnyw kwa kweli si vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…