Kuhusu kuongeza kipato

yello masai

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2016
Posts
3,662
Reaction score
3,715
Habari wakuu.

Leo nimekaa nikafikiria sana kuhusu namna ya kuongeza kipato. Hii ni baada ya kupiga hesabu za gharama za maisha hasa kwa upande wa kulipa kodi ya nyumba, nk.

Mkakati niliouona unafaa zaidi ni kuongeza kipato kwa kufungua mradi/ biashara rahisi ambayo nitakuwa na uhakika wa kuingiza faida ya tsh. 5000 kwa siku.

Hii pia inaweza kukusaidia hata wewe mwana JF katika kuongeza kipato.

Hivyo basi namkaribisha kila mwenye wazo/ ushauri kuhusu ni mradi gani au biashara ipi au bidhaa ipi unayoweza kuuza na kuwa na uhakika wa kuingiza faida ya tsh. 5000 kwa siku pengine bila kukuhitaji kuisimamia full time.

Karibuni.
 
mada nzur lkn nasikitika haitapata wachangiaji
 
Mkuu kumenyea machungwa watu, kuuza miwa nk ni kazi ngumu lakini zinalipa
 
"pengine bila kuhitaji kuisimamia full time" kuna watu wanapenda maisha rahisi aisee!!
 
watu wakusimamie wengine.. wakutafutie faida.. labda ujenge vyumba
 
Apaaa n kubet tuuu,, hakuna kaz ya kuingiza pesa umelala kama sio betting
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…