Kuhusu lockdown Rais Magufuli yupo sahihi

Kuhusu lockdown Rais Magufuli yupo sahihi

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Salamu wanaJF
katika strategies za kupambana na COVID 19 hakuna expert duniani.kila mmoja wetu ameweza kuwa na ushauri wake ambao ni valid kwa muktadha wa uelewa,taarifa,uzoefu,elimu n.k
Rais Magufuli alichagua NO LOCKDOWN ..!!

Baada ya msimamo huu hata mimi big fan wa Jembe Magufuli nilitetereka kidogo lakini kupitia tafiti zangu hatimaye nimeelewa somo vilivyo...na somo hili limeeleweka duniani kote yaani kwa wataalamu na wanasiasa.yaani lockdown sio suluhu ya kudumu kwenye tatizo linalodumu.

Kwa mujibu wa data tatizo la COVID 19 linaonekana ni tatizo sugu tutaishi nalo na sio tatizo la kupita kama ilivyokuwa kwenye matatizo yaliyowahi kuisumbua dunia hapo awali.
basing on these facts naungana na Mh Rais katika kuikataa lockdown.

Nini kifanyike kwa sasa.
1-Tuondoe hofu iliyojengwa
2-Tutengeneze vifaa kinga kwa watumishi na jamii kwa wingi
3-Tuzingatie Social and Physical distancing
4-Tuendelee kuzingatia unawaji mikono
5-Tuendelee kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima
6-Tupime wahisiwa na kutoa majibu sahihi kwa wakati.
7-Vyombo vya ulinzi na usalama hasa polisi virejee katika routine zao za kazi(hakuna kuogopa) this is just like other War
8-wataalamu wa wizara husika waendelee kufanya analysis na kutoa muelekeo.hasa wataalamu wa epidemiolojia.
9-Watumishi wa afya warejee misingi ya viapo vyao,wapongezwe,wapewe motisha.
10-Tujiamini zaidi katika mbinu zetu kupitia mamlaka zetu kama TMDA,MSD,NIMR,Taasisi za Elimu n.k
11-Tuachane na unyanyapaa na Siasa za majitaka.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Nakubaliana na wewe hakuna haja ya kuogopa kiivo ni muhimu kujikinga na maelekezo ya kujikinga na corona tumeshapewa iyo lockdown ya nini sasa......sema form 4 failure wakitoka kwenye page ya mange lazima waje kukebei apa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
kebehi ni sehemu ya maisha humu JF
 
Magufuli yuko sahihi.
Tusali sana.
Hatuna madaktari wa kutosha
Hatuna vifaa wala dawa za kutosha
Tu masikini mno kufanya chochote juu ya janga hili.
Tusali na kuomba Mungu atusaidie.
 
Mabeberu na vibaraka wao wenye mpango wa kutumia COVID 19 kumuharibia Mzee baba Jembe Magifuli wasahau kwa sababu tutakula nao sahani moja...COVID 19 ni kionjo tu kwenye mboga.
JPM is there to stay mpka nchi ikae sawa.
 
Magufuli yuko sahihi.
Tusali sana.
Hatuna madaktari wa kutosha
Hatuna vifaa wala dawa za kutosha
Tu masikini mno kufanya chochote juu ya janga hili.
Tusali na kuomba Mungu atusaidie.
'Tu masikini mno kufanya chochote juu ya janga hili.'

Nadhani hapo umekosea sana ku-type mkuu,tangu 2015/10 tumeshatoka kwny umaskini tuko kwny donor country level.
 
ID yako mpya ni ipi?Maana sasa mmefungua mpya kwa fujo sana!
 
Magufuli ameweza kuidhibiti Corona kwa 100%
Ni wakati sasa wa kuruhusu shule zifunguliwe
Wizara ya Elimu ikikaa na Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii jinsia na watoto wakikaa pamoj watapata safe way ya kufungua Shule.
 
Mabeberu na vibaraka wao wenye mpango wa kutumia COVID 19 kumuharibia Mzee baba Jembe Magifuli wasahau kwa sababu tutakula nao sahani moja...COVID 19 ni kionjo tu kwenye mboga.
JPM is there to stay mpka nchi ikae sawa.
Umeanza kuharibu tayari!Dunia sasa inataabika na Corona,wapuuzi mnakuja na ujinga sijui mabeberu,damn kwa lipi mlilonalo?Acheni siasa mufilisi!
 
Afungue shule na vyuo.. the virus is here to stay with us..

life has to go on....... kids got to go to school.
 
sijakuelewa!mmetamba sana baada ya mimi kutulia kidogo??
Umetulia au jina lako lilikosa mvuto mpaka ukasajili lingine?Jifunze kuandika hoja za maana na utaheshimika!
 
Umeanza kuharibu tayari!Dunia sasa inataabika na Corona,wapuuzi mnakuja na ujinga sijui mabeberu,damn kwa lipi mlilonalo?Acheni siasa mufilisi!
nimeweka facts tu ..zinaweza kuumiza
 
Afungue shule na vyuo.. the virus is here to stay with us..

life has to go on....... kids got to go to school.
coordinated re opening of schools.
kwa mfano tunaweza anza na kufungua vyuo vya wataalamu wa tiba(mwaka wa tano),form four,form six na darasa la saba
 
Back
Top Bottom