Kuhusu Maadhimisho ya Nane Nane Moro:Kuna Vitu Vimeniudhi Sana

Bw.Daffa

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
420
Reaction score
116
Wakuu wote!

Jana nilipata wasaa wa kutembelea maadhimisho ya sikukuu ya wakulima-Nane Nane pale Morogoro kwenye vya Mwl.JK Nyerere.

Kama kawaida watoto na vijana wa makamo(Form 1-4) ndo walikua wengi. Sasa utaratibu wa sherehe hizi kwa kweli unaboa sana.Kwanza hii tabia ya kufanya sherehe hizi kuwa kama soko la wamachinga(najua wote wanatafta rizki) sio mzuri.Nilishangaa kuona watu wengi wapo kwenye kununua viatu,miwani,nguo za mnada n.k wakati kenye bidhaa za kilimo zenyewe watu ni wachache.

Pili hili swala la kufanya Nane Nane ndio soko la kuuza mazao ya kilimo nalo sioni uzuri wake kwani nia ni kueleimisha na sio kuuza sana.Nimeshudia makundi ya kina baba na mama wanaenda tu kununua mboga na matunda,wengi hawana muda wa kuuliza hata jinsi mboga ile inavyolimwa..

Tatu,wazazi wengi wameona Nane Nane ni sehemu ya watoto kwenda kushangaa na hivyo wao hawaendi au wanawapeleka watoto wao.. kwa nyakati tofauti niliskia kina wakisalimiana na wenzao na wakisema "nimewaleta watoto bwana".. Hii ilifanya 80% ya watu wakawa watoto na School boys/girls..

Nne sisi vijana tunadharau kilimo sana.Nimeshuhudia maeneo mengi ya maonyesho yakitembelewa na wazee au vijana wakubwa(roughly with ages above 35yrs). Vijana wa kati ya 18-30yrs wengi nimewaona wakiwa wameshikana mikono na wapenzi wao na walifika kwenye maonyesha kupiga picha tu ila sio kupata elimu flani.

Tano hata wanaohusika wenyewe(Wakulima/Waelimishaji)wame jijengea imani kwamba watu wazima(wamama/wababa) ndio wanaofaa kuelimishwa.. kwa mara kadhaa niliomba kuelimishwa kuhusu Incubators,Greenhouse na nakumbuka hata kwenye kataasisi flani kakutoa mikopo walinipa maelezo kwa kifupi sana(ofcoz am 20's).. tena jamaa wa Incubators akanambia 'hizi vitu ni ghali sana'
Hii iliniskitisha sana mana inadhihirisha kwamba watu wapo pale kufanya biashara na sio kuelimisha!

Wakuu hayo ni mambo ambayo kwa upande wangu sikuyapenda mana yapo kinyume na Adhma ya maadhimisho ya Nane Nane. Pengine kuna mambo ambayo yapo sahihi ila tu sifahamu-tuelimishane. Au na nyie kama kuna mambo mliyaona basi tushirikishane..
Nadhani kuna haja ya serikali kuangalia upya utaritibu huu kwani vinginevyo Lengo litakua halifanikiwi.
 
Niliwahi sema hakuna mainyesho ni uhuni na TASO wako bise kukusannya pesa
 
We need to change, hata waelimishaji wenyewe wengi wao ni incompetent au hawako serious na yale wanayopaswa kufanyan. Wapo pale kusukuma siku ziende tu.
 
mkuu upo sawa kabisa, yani mimi nimeona kama nimechoma fedha yangu tu kwenda nanenane moro, maana hata asasi nilizozitembelea nyingi ziliweka wanafunzi wa sua, hawana uzoefu na waliyokuwa wanayaongea, yani wapo wapo tu.

pili viwanja vya nane nane Morogoro vipi kwa zaidi ya miaka 10, ila havina maboresho yoyote, pathways zimejaa kidongo chekundu, ukiingia hapo nawe watoka mwekundu.

kwa hali nliyoiona, sidhani kama serikali ipo serious na kilimo kama biashara.
 
Dah! Poleni sana wadau, nilikuwa name Nia ya kwenda Leo ila kwa mantiki hiyo hakuna haja tena!
 
Watanzania bado vna safari ndefu sana kufikia kujitambua kwa kweli
 
Jaribu ukipata pesa hudhuria maonyesho ya kilimo ya Kenya hutajutia kamwe hata kama utakuwa umetumia Milioni moja, huwezi kuta uhuni kama wa bongo huwezi kuta taasisi za serikali ya kenya zisizo husiana na kilimo, huwezi kuta bidhaa tofauti na za kilimo au ufugaji. Nilihudhuria maonyesho yao kwa kweli wako vizuri Tanzania hata sabasaba ni uhuni maonyesho yamejaa wachuuzi
 
We need to change, hata waelimishaji wenyewe wengi wao ni incompetent au hawako serious na yale wanayopaswa kufanyan. Wapo pale kusukuma siku ziende tu.
Kumbe bwana.. Kuna jamaa nilimuomba anieleze jinsi ya kujenga ghala la mbogamboga.. alianza kwa kunihoji eti Mie kwani nasoma chuo gani.. Nilishangaa sana!
 
Shukrani Mkuu.Kuna jamaa niko nae chuo yeye alisoma na kukulia Kenya haya masuala ananielezaga sana asee
 
Mimi nilihudhuria pia najiuliza zile pesa za viingilio wanafanyia nini yani wapo vululu vululu shame on them!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…