Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Kuna kitu cha msingi na cha muhimu ambacho tunapaswa kutoa kwa watu wetu. Kitu ambacho kitatuunganisha na ambacho ndiyo msingi haswa wa uwepo wa taifa lolote. Bila msingi huo, hakuna taifa ambalo litaendelea kwa muda mrefu, hata kama lina watu wenye maarifa ya kiasi gani katika uzalishaji mali na katika ugunduzi. Utambuzi huu wa mtu kwa mtu mwingine kama raia wa nchi moja, ambao wana haki na wajibu na wenye maslahi ya pamoja kwa taifa lao.
Dunia unayoiona imeunganishwa na nguvu na sheria ambazo zinailinda na kuiendesha. Tunatakiwa tuzijue kama taifa na tusienende kinyume chake.
Na hili ni maisha ya kijamii, ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa jamii yeyote ile. Pale maisha ya kijamii yanapoachwa na watu kufuata ubinafsi, na sio kuangalia jamii na maendeleo yake; na kulinda maadili ya taifa, lazima shida zitakuja tu kutukabili na utatuzi wake utakuwa mgumu.
Watu wakigawanyika kuwarudisha pamoja ni ngumu sana. Nadhani tunapaswa kubadili jinsi tunavyofikiri na kuongoza mawazo yetu na mtizamo wetu kwa taifa letu na tunavyoonana wenyewe kwa wenyewe. Kuondokana na matatizo pengine yatakayotukabili kutokana na mwenendo tunaoenda nao. Ili taifa liwe imara haina budi mahusiano yake yawe imara ndani yake yenyewe.
Ikiwa watu wamegawanyika katika mawazo na matendo hakuna kikubwa tutakachofanikiwa.
Haya yatatokea kwasababu tutakuwa tumeacha njia ambayo ni sahihi, tunayopaswa kupita, na kuchagua njia ya ubinafsi. Kwasababu hii; hatutaepuka mifarakano katika jamii na kwenye siasa zetu. Kama akili zetu ziko binded kwenye pesa, madaraka na umaarufu na haya yakawa mwongozo wetu badala ya kufocus kwenye kuleta watu pamoja lazima watu watagawanywa. Na uzalendo hautakuwepo tena.
Hila, fitna, ulaghai ikawa nguzo yetu ili kufikia malengo yetu ya kisiasa na pengine kupata umaarufu na pesa, hili taifa ambalo limefurahia amani yake kwa muda mrefu huenda ikatoweka. Lazima tukumbuke hakuna taifa litakalosimishwa imara bila misingi ya ukweli na haki. so ni wajibu wetu kufikiria haya mambo kama tunataka kujenga taifa zuri na moja. Amasivyo tutegemee..
Umoja wa kitaifa kutashuka kwa kiwango cha juu, hatuwezi kuepuka hili la umoja wa kitaifa kushuka kama kila mtu akiangalia maslahi yake binafsi. Na taifa halitoweza kuwa imara. Ulinzi wake hauwezi kuwa imara pia kwa taifa ambalo watu wake sio honest, wasio na maadili na wala sio wamoja. Maadili katika taifa ni ya msingi sana na ya kuzingatia.
Kwahiyo kama taifa hatupaswi kuangalia ubinafsi wetu bali tunatakiwa kuangalia na kujali maendeleo ya jamii zetu. Na biashara ziwe ni kwa maendeleo ya kiuchumi ya jamii husika kuliko kuweka kipaumbele katika ubinafsi.
Tuangalie kwa umakini tunapotafuta maendeleo yetu ya kiuchumi yasikinzane na ustawi wa jamii zetu. pasipo kuangalia haya mambo ya kimsingi yanayotuunganisha na ambayo ndio huleta pia ukuaji wa kiuchumi wa jamii husika kuwa endelevu hatutafika mbali.
Kwasababu pasipo kuwa wamoja na kufanya kazi pamoja hatuwezi kuendelea. Tutaendelea kama tutaacha mawazo ya kibinafsi na mawazo yetu tukayawekeza kwenye ujenzi wa taifa hili.
Tukitafuta maendeleo ya taifa letu kwa pamoja tutaendelea haraka zaidi. Na tutajenga utangamavu kwenye jamii.
Tukiangalia ubinafsi tutakuwa na jeshi ambalo linaangalia maslahi ya watawala na linalotumika kwa maslahi binafsi, badala ya wananchi na ya taifa, na tutakuwa na raia ambao hawana uzalendo na wapinzani wa serikali yao na waliogawanyika. Ambao kwao pesa ndio kitu cha msingi kwao na rahisi kununulika. Security ya nchi tutaiweka rehani. Maadili ya nchi ni ya msingi kwa taifa lolote ndiyo ambayo huunganisha watu. Na watu kijua haki za wengine.
Jamii ambayo pesa ndio msingi namba moja kuliko mahusiano yao na pesa hiyo ndiyo inayowasukuma kuingia kwenye siasa, na kwenye uongozi wa nchi, haiwezi kujenga taifa moja na bora.
Lakini pia viongozi waliofuata fedha hawataweza kujenga jamii bora pia zenye maelewano na ushirikiano.
Jamii bora hujengwa pale watu watakapofanya kazi pamoja kuimarisha maisha yao bila kuangalia ubinafsi. Hii roho ya kuhudumia wengine na kujali maisha ya wengine ndio hufanya taifa kuwa imara.
Sisi kama taifa tumetoka kwenye msingi huu. Tumekuwa taifa la ubinafsi na sio taifa la watu wanaotumikiana. Hali haijawa ya kutisha sana lakini tusipokuwa makini tutadumbukia katika shimo ambalo itakuwa vigumu kwetu kutoka.
Ukweli ni kwamba hatutaweza kulijenga taifa hili kama sisi tunaoliunda taifa hili hatupendani na kuheshimiana.
Sent using Jamii Forums mobile app