Mkuu
Mrimi, ahsante kunikumbusha hilo...anyway huko si taaluma yangu lakini natambua wapo wataalamu wengi katika forummf
MziziMkavu n.k
Nadhani kuna shida fulani hasa katika utambuzi wa uginjwa(Diagnosis) wa Malaria..yaani kwa wengine Malaria ni
-Kuwa na homa au
-Kujisikia kuchoka au
-Viungo kuuma na kwa wengine
-Kujisikia vibaya.
na matokeo yake mtu huamua kwenda duka la dawa(pharmacy) kununua dawa Bila kupima(kuwa na uhakika), kisha linakuja tatizo lingine la matumizi ya dawa..
All in all, kutopona kwa ugonjwa kunaweza kusababishwa na
-Ugonjwa unaodhaniwa(Diagnosis) si sahihi.
-Kutopewa dawa/ dozi sahihi ingawaje ugonjwa umetambulika.
-Kutokuwa makini na matumizi mazuri ya dawa( kutotumia dawa kwa wakati, kutomaliza dozi hasa mara baada ya mgonjwa kupata unafuu)
-Madawa kutofanya kazi mwilini kwa sababu ya kuzoeleka( Resistance).
Muhimu, kufanya vipimo kujua hasa tatizo liko wapi na si kujaribisha dawa kila wakati.