Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu utalamba kiasi ulichochangia tu hakuna faida vilevile usingae kwenye Statement ukakuta baadhi ya miezi mwajiri hakupeleka michango.Hakuna utakachoambulia ndugu. Pesa zishapigwa na wajanja walio madarakani kitambo.
Kama una njia mbadala za kupata pesa wewe katafute tu. Huko utaenda kupewa majibu ya shombo, mwisho wakwambie usubiri utimize miaka 55 halafu ukijiangalia kipindi hicho una miaka 25.
SawaNenda Office za NSSF ukiwa na barua ya kuachishwa kazi ama barua ya kusitishwa mkataba na mwajili wako,, ukikidhi vigezo kwa mujibu wa sheria utalipwa michango yako yote baada ya mwezi mmoja tu,, isiwe umeacha kazi mwenyewe,, narudia tena isiwe umeacha kazi mwenyewe kwa maana ya kujiuzuru,, hapa utashauriwa utafute kazi pengine na uendelee kuchangia,, vinginevyo itakulazimu kusubiri hadi utakapo timiza umri wa miaka 55,,
DuhHakuna utakachoambulia ndugu. Pesa zishapigwa na wajanja walio madarakani kitambo.
Kama una njia mbadala za kupata pesa wewe katafute tu. Huko utaenda kupewa majibu ya shombo, mwisho wakwambie usubiri utimize miaka 55 halafu ukijiangalia kipindi hicho una miaka 25.
NSSF pamoja na baadhi ya waajiri miyeyusho wafanyakazi wa reli ya mwendokasi toka January hadi sasa hawajaingiziwa michango yao.Hatari, nilijua kuna faida itaongezeka kama motisha ya kuwa mwanachama
kwa ninachofahamu kama mtu anakuwa hajawa na vigezo vya kuwekwa katika penseni kinachofanyika atapewa pesa au mafao yako kama sehemu ya mafao ya kukosa ajira,cha muhimu awe na nyaraka zote zinazoonyesha alisimishwa kazi na taratibu zingine zitafuata kwa mujibu wa miongozo ya NSSFWadau wa jukwaa salamu!
Nawasilisha swali langu hivi, kama mfanyakazi ameachishwa kazi lakini hajafikisha vigezo vya kulipwa pensheni je atalipwa tu malipo aliyochangia au atapewa na faida kulingana na michango aliyochangia?
Asanteni, nawasilisha
Asantekwa ninachofahamu kama mtu anakuwa hajawa na vigezo vya kuwekwa katika penseni kinachofanyika atapewa pesa au mafao yako kama sehemu ya mafao ya kukosa ajira,cha muhimu awe na nyaraka zote zinazoonyesha alisimishwa kazi na taratibu zingine zitafuata kwa mujibu wa miongozo ya NSSF