FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Habari zenu wakuu!
Kwanza kabisa, baada ya Marekani kupitia rais Donald Trump kutangaza kusitisha rasmi mahusiano na Shirika la Afya Duniani WHO, kunaweza kuwa pigo kubwa kwa shirika hilo maana hapo baadaye ndani ya kila miaka miwili shirika litakuwa likizikosa dola za Kimarekani takribani milioni 900, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko mchango wa nchi nyingine yeyote ile.
Lakini kabla hatujafika huko, kuna swali la kujiuliza;
Kama Trump alikusudia kuiondoa rasmi Marekani kutoka WHO katika taarifa yake hiyo Ijumaa, suala hilo likoje kisheria?
Kuna mkanganyiko!
Kikanuni, WHO haijaweka wazi kuhusu utaratibu wa wanachama kujiondoa katika shirika hilo kikatiba, suala ambalo linakwenda moja kwa moja katika Mkataba wa Vienna wa mwaka 1969 juu ya Sheria za Mikataba ama kwa lugha nyingine Vienna Convention on the Law of Treaties.
Hapo sasa Marekani itahitajika kutoa notisi ya miezi kumi na miwili (12) kabla ya kujitoa rasmi WHO, chini ya huo Mkataba wa Vienna wa mwaka 1969, unaodhibiti mikataba ya kimataifa.
Maana yake ni kuwa, Marekani bado ni nchi mwanachama wa Shirika la Afya Duniani WHO kulingana na sheria ya kimataifa pamoja na Trump kutangaza kuvunja mahusiano na shirika hilo saa kadhaa zilizopita.
Pia,
Mnamo mwaka 1948 wakati Marekani inajiunga WHO, bunge la Congress nchini humo lilipitisha azimio kwamba nchi hiyo yaweza kujiondoa katika ushirika kwa notisi ya mwaka mmoja, ambalo lilikubaliwa na Shirika la Afya Duniani WHO.
Maana yake ni kwamba, rais Trump anao uhalali kisheria wa kuiondoa Marekani kutoka WHO bila idhini ya Congress lakini kutokana na azimio lililopitishwa na bunge hilo, Trump atalazimika kusubiri mwaka mmoja kabla ya kufanikisha azma yake kama kweli anahitaji kuiondoa Marekani kutoka WHO.
Hivyo basi si jambo la ghafla tu kutangaza kujiondoa bali ni suala lenye mlolongo mrefu kisheria ama kinyume na hapo tunaweza kusema kuwa Trump hakukusudia kujiondoa WHO kama watu wanavyodhani ama alinukuliwa vibaya jambo linaloibua maswali mengi.
Kinachoonekana kwa sasa ni Marekani chini ya Trump kusitisha ufadhili ama fedha kwa shirika hilo katika kipindi cha muda usiofahamika na si jambo la kujiondoa kabisa uanachama wa shirika hilo kwa sasa. Asante!
Karibu kwa maoni!