Raelish
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 489
- 162
Habarini humu, Kuna tetesi ambazo zinaonekana kama ni kweli hivi. Kwamba mwaka huu vyuo vya afya ngazi ya cheti na sitashahada kutakuwa na mitihani ya Taifa kutoka nacte., ila mpaka sasa ratiba hazijafika vyuoni ila inasemekana mitihani itaanza tarehe 3 agosti, kwa wale ambao wapo karibu na nacte au wenye taarifa kamili watujuze, ila ikumbukwe tayari Wanachuo waliambiwa walipie mitihani hiyo Tsh laki moja na nusu na tayari fedha hizo zimelipwa. Karibun kutujuza jamani.