Kuhusu mwanasheria wa familia, ni kila familia inahitaji kuwa naye?

Kuhusu mwanasheria wa familia, ni kila familia inahitaji kuwa naye?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Wakuu!

Naomba nijifunze hapa na wenzangu, maisha ya kila siku yanaongozwa na sheria. Iwe ni sheria za asili, au hizi sheria za kikatiba.

Ni kawaida kusikia familia fulani, acha kampuni, ina mwanasheria wake. Bila shaka ni mtatuzi kwa mambo ya kisheria, ila naomba nijue machache kumhusu.

1. Kwa shughuli za kila siku za familia (ukiacha mirathi na talaka ambazo ni endings) anahusikaje?

2. Anakuwa wa familia moja pekee au anaweza kusimamia familia kadhaa?

3. Ni zipi sifa za familia kuhitaji mwanasheria?

4. Kama sio mtu wa matukio.....

5. ..................

Karibuni tujifunze, wengine wataongezea.

Ncha Kali.
 
Kuna kiasi cha pesa ujishafikia utahitaji tu mwanasheria, accountant,doctor, etc wa familia.
Ukiona huoni uhitaji wake au kama wewe hapo maswali mengiii ujue bado pesa yako ndogo sana
 
Kuna kiasi cha pesa ujishafikia utahitaji tu mwanasheria, accountant,doctor, etc wa familia.
Ukiona huoni uhitaji wake au kama wewe hapo maswali mengiii ujue bado pesa yako ndogo sana

Umejibu kisheria au kihisia zako tu mkuu!

Hata hivyo nilitenganisha familia na kampuni, huyo ‘accountant’ wa familia naye vipi?
 
Wakuu!

Naomba nijifunze hapa na wenzangu, maisha ya kila siku yanaongozwa na sheria. Iwe ni sheria za asili, au hizi sheria za kikatiba.

Ni kawaida kusikia familia fulani, acha kampuni, ina mwanasheria wake. Bila shaka ni mtatuzi kwa mambo ya kisheria, ila naomba nijue machache kumhusu...
1. Kazi yake ni kuishauri familia kuhusu mambo yote ya kisheria, chochote kile kwa jicho la kisheria;

2. Anaweza kuwakilisha familia zaidi ya moja, ni yeye tu kama ana nafasi;

3. Iwe na uwezo wa kumlipa ada yake ya kuiwakilisha familia (retainer);
 
Back
Top Bottom