Old Moshi ni shule nzuri sana, binafsi nimesoma pale kuanzia form 1 mpaka 6 na imenitoa kimaisha kwani nilimaliza vizuri level zote na kwa maksi nzuri sana, kikubwa kumbuka pale ni zaidi ya chuo hamna atakaekufwatilia, unaruhusiwa kwenda mjini tena na nguo safi na muda mwingi utaona watu wa kila namna kuanzia wanaopenda starehe mpaka wanaopenda kusoma kwa bidii na wanaopenda dini sana. Kama umechaguliwa comb ya science kuna maabara nzuri zenye kila kifaa kinachotakiwa na ni bidii yako tu kuvitumia, nakumbuka form 5 ukifika hutapata kitanda mpaka form 4 waondoke so itabidi ubebwe na dogo yeyote na hilo shule haitakuambia zaidi ya kukupangia bweni then utajijua mwenyewe. All the best dogo na nimekumbuka mbali sana.