Kuhusu QR code

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Habari wakuu.

Naulizia ni wapi nitaweza kupata huduma ya kutengenezewa QR Code kwenye business card hapa Dar

 
Mimi sipo Dar es Salaam lakini naweza kuifanya kazi yako kwa ufanisi unaotarajiwa. Nimekuwa nikifanya kazi na watu toka sehemu tofauti tofauti kwa kutumia mawasiliano ya simu na barua pepe (eMail). Hivyo ikiwa upo willing, karibu tufanye kazi.

Hii ni sample ya Identity Card niliyo-design kwaajili ya partners na attendants wa Airtel Njombe, ambayo ina QR CODE - utofauti ni kwamba wewe unahitaji Business card ambayo inawezekana kwa 100%.

Gharama yangu ya ku-design business card ni TZS 5,000/= tu. Hii haihusishi gharama ya ku-print, utaprint mwenyewe hapo hapo Dar es Salaam kwasabu printers wako wengi na kwa hiyo wana gharama nafuu sana.

PROCESS:
1. Unanitumia specs na preferences (rangi, info za kuweka n.k) za Business cards zako.
2. Unalipia kwa mobile money.
3. Na-design first draft - nakutumia. Unaipitia na kupendekeza marekebisho. (Naruhusu marekebisho mpaka mara tatu)
4. Na-design final draft kisha nakutumia Business card ikiwa imekamilika kwa namna unayoitaka.
[Nakutumia file lenye PDF, TIFF, PNG, JPG na source file (PSD/ Ai - inategemea nimetumia program ipi) kwa email.]
*Turnaround: Saa 1 mpaka masaa 3 kutegemea na spidi yako ya ku-respond.
5. Tunafunga biashara kila mmoja akiwa satisfied.

Interested? Nicheck DM.


 

Salaam mkuu..

Nje ya mada, Naomba kufahamishwa hii QR code ina matumizi gani kwenye hiyo business card.

Natanguliza shukraan.
 
Salaam mkuu..

Nje ya mada, Naomba kufahamishwa hii QR code ina matumizi gani kwenye hiyo business card.

Natanguliza shukraan.
Simply, QR kazi yake ni kuhifadhi taarifa.

Utauliza taarifa gani?
Well, katika QR code unaweza kuweka url links, email, geo coordinates, na maandishi yenye taarifa tofauti tofauti.

Kwanini mtu aweke taarifa kwenye QR code?
Japo QR code ni bora kuliko Barcodes, lakini zote ni njia rahisi, zinazoaminika na za haraka za kutoa data kwa matumizi tofauti tofauti.

SASA, KAZI YA QR CODE KWENYE BUSINESS CARD NI NINI?

1. Unaweza kuweka TANGAZO kwenye QR code. Kwa mfano; unaweka link ambayo mtu aki-scan inampeleka moja kwa moja kwenye video yako iliyopo Youtube ambayo ni tangazo la biashara/ huduma/ bidhaa/ taasisi yako n.k.
2. Kuweka QR Code kwenye business cards zako kunampa mpokeaji 'options' nyingi za kumfanya aku-follow. Mfano, unai-link QR Code kwa kila account yako ya mitandao ya kijamii.
3. Mara nyingi watu huwa wana-scan kadi halafu wanaitupa (Au wanaipoteza). Ukiweka QR Code unaongeza uwezekano wa watu wengi kuona taarifa/ video/ website/ sales pitch yako kupitia simu zao.
4. Business card ni njia ya kawaida ya kubadilishana mawasiliano. Ukiweka QR code unaibadilisha kadi yako kuwa 'marketing agency' yako.
5. Ile tu kwamba umeweka picha yako na QR code kwenye business card, watu watapata msukumo wa ku-scan business cards zako (Wengi wao wata-scan kwasababu tu ya 'curiosity' - waone hiyo QR Code yako ina kitu gani?).
6. QR codes zinaweza kubuniwa (“zikarembeshwa”) na logo yako ikiwa katikati na hivyo kukuachia uwanja mpana wa kuweka taarifa nyingi katika business card yako ikiwemo kuweka QR Code zingine... kwani nani kasema lazima iwe moja?
7. Taarifa zote ulizoziandika kwenye Business card yako unaweza ukaziweka kwenye QR Code moja tu. Kwahiyo, mtu badala ya kusoma, ana-scan tu halafu anazipata taarifa zote ulizoweka.

Nimejitahidi kujibu kwa kadri ya uelewa wangu. Tusameheane pale nilipoteleza.

Naomba kuwasilisha
 

Aisee shukran sana mkuu, usipoelewa hapa basi hutaweza kuelewa popote pale!

Mkuu ukipaji cha ufundishaji, Honestly.. I appreciate.

Far away naomba kupata no yako ya mawasiliano... Natazamia kupata huduma yako.
 
Aisee shukran sana mkuu, usipoelewa hapa basi hutaweza kuelewa popote pale!

Mkuu ukipaji cha ufundishaji, Honestly.. I appreciate.

Far away naomba kupata no yako ya mawasiliano... Natazamia kupata huduma yako.
Shukrani sana mkuu. Karibu anytime; +255 627 068 027 au daisyagencytz@gmail.com

Ukiscan mojawapo kati ya QR Codes hizi hapa chini - utapata link ya INSTAGRAM PAGE yetu. Lengo ni kuonesha kuwa 'QR Codes zinaweza kuwa za style tofauti tofauti' kulingana na brand yako.

Mimi.. ninashukuru.





 
Duuh shule kubwa hii sana tu
 
SAMPLE
*Note: Website na Location ni kwaajili ya 'demonstration' tu - NOT VALID.*





BACK SIDE





🙏 Mimi.. ninashukuru.
 
Mkuu naomba kuuliza, Kama mtu anaanzisha bidhaa ya kuuza madukani, huwa nasikia ni lazima uwe na barcode, je hi inaweza kuwa mbadala na barcode, mamlaka inazitambua? Halafu je barcode zinakazi gani unawezatupa abc, (tunaziskiaga tu)
 
Mkuu naomba kuuliza, Kama mtu anaanzisha bidhaa ya kuuza madukani, huwa nasikia ni lazima uwe na barcode, je hi inaweza kuwa mbadala na barcode, mamlaka inazitambua? Halafu je barcode zinakazi gani unawezatupa abc, (tunaziskiaga tu)

NATENGENEZA BIDHAA NA NATAKA KUANZA KUUZA MADUKANI, JE - NI LAZIMA NIWE NA BARCODE (Msimbomilia)?
Sina uhakika kama ni lazima kwa mtu anaetaka kuuza bidhaa zake locally, lakini nafahamu ni 'lazima' kwa mtu anaetaka kuuza bidhaa zake kimataifa.

KWANI BARCODES (MISIMBOMILIA) ZINA KAZI GANI KATIKA BIDHAA?
Kimsingi Barcodes zinawezesha 'traceability' ya bidhaa na hivyo kurahisisha biashara. Ipo taasisi ya kimataifa inayoitwa GS1 ambayo jukumu lake ni kutoa msimbomilia (barcodes). Kuanzia mwaka 2011, Tanzania imekuwa mwanachama wa GS1. Pamoja na kutoa barcodes, GS1 pia inatoa huduma ya ufatiliaji (traceability) wa bidhaa kutoka kwa mzalishaji hadi kufika kwa mlaji. Tanzania kuna ofisi za GS1 pia || GS1 ||.

Barcode inatoa taarifa kuhusu WAPI BIDHAA IMETENGENEZWA na MALIGHAFI ZILIZOTUMIKA KUTENGENEZA BIDHAA HUSIKA (Yaani contents/ingredients). Pia barcodes zinasaidia kudhibiti bidhaa bandia na zile zilizo chini ya kiwango (Counterfeit & substandard goods). Kwa upande mwingine inarahisisha utunzaji wa taarifa kwa wamiliki wa maduka.

Kwahiyo, bidhaa yako ikiwa na barcodes inakuwa ni rahisi kupenya sokoni; kuanzia masoko ya ndani, ya kikanda na ya kimataifa. Wazungu wanasema barcodes zinaongeza 'credibility' - kwasababu ni ngumu mtu (hasa watu wa ughaibuni) kununua bidhaa ambayo haieleweki imezalishwa wapi na kwa ingredients zipi. Kwanza hata mamlaka mbalimbali za udhibiti za nchi husika zitakuwekea ugumu sana katika kukupatia vibali.

JE, QR CODES ZINAWEZA KUWA MBADALA WA BARCODES? NA VIPI MAMLAKA, ZINATAMBUA QR CODES?

Ndio, QR CODES zinaweza kuwa mbadala wa barcodes, inategemea na mahitaji. Hapana, mamlaka hazitambui rasmi matumizi ya QR CODES. Chukulia QR CODES kama cryptocurrencies hivi... zipo na zinapata traction lakini hazitambuliki rasmi. And by the way kirefu cha QR CODES ni QUICK RESPONSE CODES. Ulikuwa hujui, sasa unajua.

Well, kinadharia... narudia tena 'kinadharia' - Barcodes zimekuwepo tangu miaka ya 1940 lakini teknolojia ya kuwezesha barcodes kuanza kutumika katika maisha ya kila siku imekuja katika ya miaka ya 70 hivi. Wakati QR CODES zimeingia katikati ya miaka ya 90 hivi. Leo hii kwa kutumia simu yako tu unaweza ku-scan barcode.

TOFAUTI YA BARCODES NA QR (Quick Response) CODES NI IPI?
Hapo zamani za kale ilikuwepo barcode, njia nzuri ya kufuatilia bidhaa na kutunza taarifa iliyokubalika duniani kote. Tatizo ni kwamba binadamu tukiona kitu ni kizuri basi huwa tunataka tupate kizuri zaidi, kisafi, chenye nguvu zaidi ya kile kilichopo.

Mara paap, QR (quick response) code huyu hapa akaingia miaka ya 90. Na QR code ilibuniwa na kampuni ya Kijapani inayoitwa Denso Wave na QR code ilitengenezwa kufanya kitu ambacho barcode ilifeli; kuhifadhi taarifa nyingi zaidi. Tazama bidhaa yoyote, utakuta ina barcode... vimstari fulani simple na rahisi kusoma - lakini ubaya ni kuwa vile vimstari haviwezi kuhifadhi taarifa nyingi.

QR codes, kwa upande mwingine, zina urefu na upana, na hivyo zina uwezo wa kuhifadhi taarifa nyingi tena zilizopangiliwa vizuri. Barcodes zinasomeka kutoka kushoto kwenda kulia tu na si vinginevyo, wakati QR codes zinaweza kuhifadhi taarifa kwa mwelekeo tofauti tofauti (kutoka juu, kutoka chini, mbele yake n.k)

INA MAANA QR CODES ZINAFAA ZAIDI KUWEKWA KATIKA BIDHAA?
Turudi kwenye msingi. Kwani mfanyabiashara anahitaji nini anapo-scan code? Jibu ni QUICK PROCESSING; njia rahisi inayomwezesha kuhifadhi code ndefu ya bidhaa katika system yake ya bishara pasipo kugusa keyboard.

Barcodes na QR codes zote zinaweza kufanikisha hilo, lakini barcodes ni cheap, universal, na mara nyingi huwa zinakuwa pre-printed. QR codes zenyewe si rasmi sana na bado haziongezi thamani machoni pa wateja ukilinganisha na barcodes.

Zaidi ya yote, barcodes zina faida fulani kiufundi.

Kwasababu ya 'complexity' na uhitaji wa 'photographic reader', QR codes zina 'effective rang' ya takribani mara 10 ya ukubwa wake. Yaani kwa mfano, QR code yenye ukubwa wa inchi moja inaweza kuwa scanned kutoka umbali wa inchi 10.

Barcodes zina range kubwa sana, kwasababu ya simplicity yake na kwa ukweli kwamba zinaweza kuwa scanned kwa kutumia 'lasers'. Kuna scanner zinaweza ku-scan barcode kutoka umbali wa futi 54! Maana yake ni kwamba - ukiwa na bidhaa stoo zina barcodes, hutahangaika kupanda na kushuka ngazi ili ku-scan stock yako na vile vile inakuwa rahisi ku-scan bidhaa walizonunua wateja wako na kuwatoa fasta pasipo kuhangaika kubadilisha 'settings' za scanner.

BOTTOM LINE
Unaonaje, Barcode Vs Quick Response code nani mshindi?

Naomba kuwasilisha.
 
kwakweli mkuu nashukuru kwa darasa, nimejifunza mengi, nilitamani ziwe zinafanana ili tufanye kazi Mana nimeingiza bidhaa sokoni ndio nikakutana na hili la barcode Kama QR bado haitambuliki itabidi nitafute Kwanza barcode halafu nikiisha jiweka vizuri mitandao ya kijamii nitakutafuta tuweke taarifa hizo kwenye QR, namba yako nimesave
Shukrani
 
Sawa mkuu, karibu sana anytime.
 
Sasa Mimi mwenye simu yangu na internet au computer how do I scan the QR code?
Mfano ulioitoa hapo juu nicheki insta page yako. How do I scan?
Napiga picha hiyo code?
 
Ofisi za kutengeneza bar code ili bidhaa uende supermarket kwa hapa Dar iko wapi? Na ni shs ngapi roughly. Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…