Kwanza ieleweke wazi kwamba kazi kubwa ya serikali katika uwanda wa biashara ni KURATIBU, KUWEZESHA NA KUTOA MIONGOZO NAMNA BORA YA UWEKEZAJI kwa wafanyabishara wazawa na wageni kutoka nje.
Tanzania kuingia kununua mabehewa na ndege kwa ajili ya kufanya biashara ya usafirishaji naona ni UBADHIRIFU WA RASILIMALI FEDHA KIDOGO ambazo nchi inazo.
Fikiria zaidi ya billion 100 imeshatumika kununua mabehewa hayo huku wadau wengi wakidai hapo nchi imepigwa kutokana na kununua mabehewa ya mtumba (used).
Ombi langu serikali ingejikita kujenga reli tu ya SGR huku ununuzi wa mabehewa na uendeshaji wa biashara hiyo ya treni ingeachia sekta binafsi kwa ubia wa miaka kadhaa. Faida ya jambo hilo serikali isingekutana na hasara za mara kwa mara kutokana na gharama za uendeshaji wa mradi. Serikali ingejihakikishia kupata faida kutoka kwa wawekezaji ambao ndio wangekuwa wana mabehewa yao ya kisiasa kwenye reli hiyo.
Serikali ingeachana na ununuzi wa mabehewa kwa watu binafsi nadhani mpaka sasa ujenzi wa SGR ungekuwa umekamilika hadi Mwanza ambapo ujenzi una sua sua hadi hivi sasa.
Japo ujenzi wa SGR hii ndefu kutokea pwani hadi Mwanza na kuelekea kigoma kuziunganisha nchi za Rwanda, Burundi na DRC tumezingua kama nchi kwa sababu mchina anatucheka na kufurahia mawazo yetu mafupi. (Hii inaitaji thread nyingine ni wapi kama nchi tumezingua kwenye huu ujenzi wa mradi huu).
Sasa turudi kwenye gharama kubwa za ununuzi wa mabehewa ya sgr. Kama tunavyojua serikali imetumia na inaendelea kutumia gharama kubwa kuagiza na kuendesha mradi huu wa sgr ambapo mimi nina shauri serikali ingeanchia sekta binafsi uendeshaji wa mradi huu na yenyewe ikajikita kwenye vipaumbele vingine vya kukuza uchumi wa mtanzania mmoja mmoja.
Sasa mimi ningekuwa kwenye kamati ya ushauri wa jambo hilo, ningeshauri serikali ijikite kwenye kuendeleza sekta ya kilimo na ufugaji kwa uwekezaji mkubwa.
Sote tunakubaliana kwamba sekta ya kilimo na ufugaji kwa Tanzania inahusisha zaidi ya 70% ya watanzania wengi waliojiajiri huko. Hivyo serikali kuongeza uwekezaji kwenye sekta hiyo ni kwamba imegusa maisha na uchumi wa watanzania wengi mmoja mmoja.
Kwa namna gani mimi pesa hizo za mabeweha ningezielekeza kwenye sekta ya kilimo na ufugaji.
Ni kwa kutumia rasilimali maji ambayo Mungu ametuzawadia kama nchi kwa ajili ya kufanya kilimo cha umwagiliaji.
Wewe fikiria tuna maziwa makubwa kama Victoria, Tanganyika na nyasa halafu hatuna skimu kubwa ya umwagiliaji kutoka kwenye hayo maziwa.
Fikiria nchi kama Misri, maji baridi mengi wanategemea kutoka kwenye mto NILE ili uzalishaji wao katika kilimo ni usipime, sisi kama nchi tunafeli wapi kuanzisha mifereji mirefu ya maji kutoka ziwa Victoria kwa mfano kwenda hadi mashambani mkoani MARA, SIMIYU, SHINYANGA, GEITA hadi Tabora.
Kwa hivyo mimi ningesisitiza hizo pesa za mabehewa ziende kwenye upanuzi wa kilimo cha umwagiliaji kwa mikoa yenye potential ya kuzalisha mazao ya kibiashara ili kilimo kiwe ni kwa mwaka mzima.
Lakini pia, serikali ina haja ya kupunguza anasa (matumizi yasiyo ya lazima) kama gharama za safari, vikao na ma V8 ili kupata uwekezaji wa maana kwenye sekta ya kilimo na ufugaji.
Kwa kuacha kununua mabehewa ya SGR, serikali ingeweza kuagiza zaidi ya trekta 200 za kilimo na uvunaji kwa ajili ya mapinduzi ya kilimo (Agrarian revolution).
Tukumbuke hakuna nchi yoyote tajiri duniani iliyofika kwenye mapinduzi ya viwanda pasipo kupitia kwanza mapinduzi ya kilimo.
Hivyo serikali itafakari sana kwenye uwekezaji wa kununua mabehewa ya sgr kwa pesa hizi za madafu huku uchumi wa watanzania wengi ukizidi kuwa dhoofu lihali.