Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 772
- 2,421
Nilikuwa namsikiliza katika kipindi cha sports arena Mwina Kaduguda akizungumza kuhusu swala la Meddie Kagere kupata nafasi hafifu ya kucheza kwa siku za hivi karibuni. Mashabiki wamekuwa wakilalamika inakuwaje the best striker anakosa nafasi katika kikosi. Point kubwa aliyoizungumza ni Afya ya mchezaji (Kagere). Kaduguda anasema kuwa Simba kwa kushirikiana na FA ya Rwanda walifanikisha matibabu ya Meddie Kagere. Timu ya taifa ilifanikisha kagere kupata nafasi ya kutibiwa ufaransa na simba ikagharamia matibabu yote.
Na ushauri wa daktari ulionesha kuwa Kagere anatakiwa kupewa muda mfupi uwanjani hadi hapo atakapokuwa tayari kucheza dakika 90 (full recovered). Hii ndio sababu ya meddie kagere kupewa muda mfupi kwenye mechi ya plateau kwasababu bado hajapona sawia na simba haitaki kutake risk. Cha kushangaza, baada ya matibabu timu ya kwanza kumtumia kagere ni timu ya taifa ya Rwanda. Akiwa kule amecheza mechi za timu ya taifa na nyingine amemaliza dakika 90.
1. Inakuwaje Timu ya taifa wamchezeshe dakika nyingi huku wakijua ushauri wa daktari hauruhusu hivyo?
2. Inakuwaje Simba hawajalalamika kuhusu mchezaji wao kuchezeshwa dakika nyingi tofauti na ushauri wa daktari?
3. Kama swala lilikuwa ni kutibiwa nje ya nchi, na kama simba ilikuwa na uwezo wa kugharamia gharama zote za matibabu, ilishindikanaje wao wenyewe kumpeleka nje ya nchi bila kushirikiana na FA ya rwanda.
4. Inawezekanaje simba watumie gharama kumtibu mchezaji na wala wasichukue hatua zozote dhidi ya timu ya taifa kwa kurisk kumchezesha mchezaji muda mrefu kinyume na ushauri wa daktari?
Kuhusu swala la kagere kuanza kwa kucheza dakika 90 kule Rwanda baada ya kutoka kwenye matibabu halafu hapo hapo Simba wanampa dakika 15 kufata ushauri wa madaktari, Kaduguda anasema pengine falsafa za walimu (Simba na Rwanda) zimetofautiana. Je, ni faslsafa gani zisizoheshimu ushauri wa madaktari? Hii ni sawa na kunawa baada ya kula.
Kaduguda umeongea, tumeskusikia ila tumeshindwa kukuelewa. Maswali ni mengi sana.