Kuhusu suala la watoto kupotea, kuna mtu anatakiwa kuwajika

Kuhusu suala la watoto kupotea, kuna mtu anatakiwa kuwajika

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
1. Waziri
2. IGP
3. DG wa Teeth
4. Sa100 mwenyewe
5......n.k

hivi kweli wameshindwa kukamata mzizi wa hiki kitu hadi wananchi wachukue sheria mkononi? samia ameona yule mzanzibari mwenzie mambo ya ndani anatosha sana kwenye mazingira kama haya kiasi kwamba nape na makamba ndio walishindwa kazi kuliko huyu jamaa? kweli? kweli?

Nchi ina jeshi, ina polisi, ina usalama wa taifa, ina kila kitu, wanapokea mishahara ya kodi za wananchi, halafu watu washindwe kufanya hata kazi wanawaza watoto wao wasijetekwa?

Juzi hapa kuna clip ya mtoto wa Kitanzania miaka kama 5 wa kike alikamatwa na polisi malawi, ametelekezwa, anasema kuna mtu alimchukua hajui anampeleka wapi.

Jana South Africa wameonyesha clip mafurushi ukilifungua kuna mtoto mzima kajikunja anasafirishwa kama magimbi kwenye salfeti, INASEMEKANA WANAPELEKWA KWENYE UCHIMBAJI MADINI HUKO KWA MADIBA, wengine wanaondolewa viungo na kuuzwa, wengine wanatolewa makafara ya kuchinjwa n.k

Inakuwaje hii issue iwe kubwa Tanzania ila Kenya, Uganda, Malawi, Zambia haipo? Tanzania kuna nini, uchochoro gani au na ninyi ni wahusika mnaona msijewachongea watu wenu?
 
yaani ukachero wanaoujua hawa sio kwenye mambo kama haya. ni kwenye kutafuta wapinzani, kuteka na kupeleka watu mbuga katavi,ila kuweka makachero au hata kujumuisha intelijensia ya wananchi wa kawaida kabisa, mnashindwaje?

jana hapa clip inazunguka katoto ka miaka 16 kanasema kameteka watoto wawili na wametumwa na MZEE SAID hapahapa DSM, hivi samia mjukuu wake au mtoto wake angetekwa mbona siku hiyo hiyo tungekamata vyanzo vyote vya utekaji, mnafanya kazi kwa ajili ya nani sasa kama sio kwa aajili ya wananchi?
 
Tuna viongozi wa ovyo sana na hili tatizo linaanza kwenye ngazi ya familia,

kutokuwajibika, tamaa za mali, selfishness, uvivu, rushwa n.k hizi tabia hazimpati mtu akiwa ukubwani ni matokeo ya malezi mabaya kutoka utotoni
 
Siku akipotea wangu...Tanzania nzima mtajua...uzembe kama huu kamwe sitaweza vumilia...
 
Ndugu wananchi tuwajubike katika hili hasa maombi na ushirikiano mzuri na jeshi la JWTZ
 
you just imagine, haya yote yanatokea, ila kuna polisi, kuna TISS, kazi yao nini? yaani nao wana hofu kama walivyo wananchi tu nao wanaogopa watoto wao kutekwa na hakuna wa kukamata hao watu wakati wao ndio wenye mabunduki, wenye maintelijensia na kila kitu. hivi kipindi cha magufuli utekaji kama huu ungekuwepo na watu wakawa wanachekacheka tu huko maofisini kweli? halafu huyu waziri wa mambo ya ndani, kwanini huwa wanampa uwaziri, alishawahi kuweza kazi wapi?
 
Mkuu umeandika kwa hasira sana. Kweli hili suala lifuatiliwe kwa kina
chukulia picha, mtoto anacheza mtu anaruka ukuta anamteka, au mtoto anaenda dukani mtu anamteka, au mtoto anatoka shule mtu anamteka, mtoto mwenyewe ni miaka midogo kabisa, trauma anayoipata kuna hakuna baba wal amama around, kuna wauwaji, hajui anapelekwa wapi, hajui yupo wapi, hajui kinachoendelea, kama vyombo vya dola vimeshindwa kuwakamata, si waachie ngazi watu wengine wachukue nchi? kazi yao ni nini sasa? au wamesalenda.
 
Nimejiuliza hivi wale jamaa wa mkiru kipindi cha JPM ndo wangetokea sasa hivi si ingekua tunakimbia nchi jirani kutafuta hifadhi😎.Sasa hawa wajinga 2anachukua watoto wetu wanachukuliwa watu wazima kiongozi mkubwa anakuja anasema ni drama ...ama ndo mhusika mkuu nimeishia kujuta tu kua mtz
 
Back
Top Bottom