Kuhusu tatizo la Programmer kuwa wachache bongo

Kuhusu tatizo la Programmer kuwa wachache bongo

jikuTech

Senior Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
108
Reaction score
159
Kuna mtu alisema ukitaka kutatua tatizo kubali kwanza kwamba lipoo

Na hili ni tatizo tayar lipo

Nije na ushahidi kwamba mfano huko nchi kama marekani watu hawa somi hii taaluma ili kuajiliwa na serikali kwa asilimia kubwa
Wanasoma kozi hii ili kuajiliwa na makampuni binafsi kama Google, Facebook, Tesla, na makampuni mengine ambayo hatuyajui

Kitu kinachofanya wanafunzi kutafuta elimu bora inapatikana wapi haijalishi ni serikalini au ni Udemy au ni street code camp ili tu kuwa na viwango kama vinavyo hitajika na makampuni na sio taasisi za serikali

Kitu kina pelekea hata vyuo vya kiserikali ku shape mutaala yao kwa mahitaji ya makampuni au kulingana na wakati

Na bila kufanya hivyo huenda wanafunzi wangekuwa wachache kwenye vyuo hivyo

Na hata interview zao ni tofauti kidogo

Kibongo wanatazama vyeti tu , na siyo uwezo wa mtu japo cheti ndio ushahidi wa uwezo wa mtu ili vyeti vya kibongo ubora wa mtu upo wa aina 2


Ushauri wangu kwa yeyote alinufaika na TEHAMA asiache kutoa ushuhuda hadhalabi ili angalau kuamsha ufuatiliaji wa habari hizi kwa watu wengine wanaotamani kuingia huku

Mimi ni Programmer niliye jitengeneza kwa msaada wa bando la Internet

Na Sasa ni Mwalimu wa Development kwa kiwango cha PHP, MYSQL NA JAVA kwa watu wanao jitambua tu.

yaan Web Development na Android Development

Huwa napatikana jwa namba 0682329852 masaa 24


Ukiwa kwenye google ukaandika Jiku Tech Tips utaona content zangu kutoka platform mbalimbali


Mimi yangu ni hayo
 
Ulienda chuo? Ulikuwa na elimu gani ya msingi kukuwezesha programming kwa msaada wa Internet?
 
Nilijifunza matumizi ya internet kwanza
Nikatumia muda mwingi kujifunza mambo mengi ya namna ya kunufaika mtandaoni
Nikaona habar ya kumiliki website, kununua sina uwezo nikajifunza html kama week 4 nikachoka nikaaacha

Nikaona kuna suala la kununua hosting siliwez
Nikahamia c nikajifunza sana
Nikaona implementation yake ni ngumu

Kila kitu hapo juu nilikuwa na soma theory

Nilivyo pata kuwa na kompyuta nikaanza na java

Kuna YouTube channel moja inaitwa freevodecamp niliangalia sana tutorial zao zile ndefu ndefu nilitumia gharama kubwa sana kwenye kununua bando.


Nilitumia muda mwingi nikiangalia tutorial zile code anazo kuwa anaziandika mfundishaji kwenye computer yake nakuwa naziandika kwenye daftari zote daftari likijaa na pause video naenda kununua lingine nikimaliza naingia kwenye IDE mara yakwanza zilikuwa hazileti majibu mara siku moja majibu yakaja kama ya mfundishaji nikafurahi sana

Tangu siku hiyo nikaacha kuandika nikawa nafungua IDE na video kwa pamona nakuwa na practice

Nikaacha kuangalia video

Nikatafuta website

Moja inaitwa geekforgeeks.com,javatpoint.com, w3school.com



Nikaja kugundua kumbe programming sio peke yangu ninaye pitia changamoto yaan bugs kumbe kuna sehemu watu wanna share matatizo yao na yana jibiwa na walio tangulia site hiyo inaitwa stackoverflow.com ni site maarufu self taught yoyote lazima anaifahamu na hata ambaye sio self taught

Nikapata ujasiri hadi wa ku edit full project ya mtu naifanya ninavyo taka

Yaan naweza chukua source code nikatengeneza products nyingi kutoka kwenye hiyo


Baada ya hapo nikawa na uwezo wa kufikilia na kutenge eza program kama niliyo waza

Baada ya hapo nikawa na uwezo huu wa kuangalia au kusikiliza tatizo la mtu na kutengeneza kwa kadri anavyo taka


Yaan kiufupi mimi ni DEVELOPER WA VIWANGO VYANGU


0682329852

KWA swali lolote la ufahamu au challenge yoyote kuhusu development
Masaa 24
 
Back
Top Bottom