ellyseniour
Member
- Dec 27, 2016
- 30
- 11
Nimekua nikisikia mara kwa mara wachambuzi mbalimbali hasa katika vyombo vya habari ikiwemo Televisheni na Radio wakichambua kuhusu mada za ukuaji wa lugha ya Kiswahili kama vile kuongezeka kwa misamiati na maneno mengine mengi ambayo wao wamekua wakiyaita maneno ya mtaani au maneno yasiyo rasmi imefikia mahali hata wachambuzi hawa kuona kwamba Kiswahili kinaharibiwa au hakitendewi haki kutokana na maneno hayo.
Wakati nasoma Kiswahili sekondari mwalimu wangu aliwahi kunifundisha kuwa ili lugha ikue na baadhi ya maneno kusanifiwa na kutumia rasmi nilazima yaibuliwe na jamii na kutumika ndio haya maneno tunayaita misimu. Ambapo kama yatadumu kwa muda mrefu na kutumika katika jamii yanaweza kurasimishwa na kuwa maneno rasmi ya Kiswahili na tukumbuke ili lugha ikue ni lazima iongezeke misamiati. Sawa swali langu ni kwa hawa wachambuzi ambao wamekua wakibeza maneno ya Kiswahili ambayo yamekua yakizuka na kutumika na wanajamii wakiona yakawa ni uharibifu wa lugha je wako sahihi kweli...?
Inamaanisha hawajui kwamba maneno haya baadaye huweza kusanifiwa na kuwa lugha rasmi...?
Naomba kuwasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app