Uchaguzi 2020 Kuhusu wagombea kuchukua, kujaza na kurejesha fomu

Uchaguzi 2020 Kuhusu wagombea kuchukua, kujaza na kurejesha fomu

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Hii inawahusu wagombea wote, katika ngazi zote kutoka vyama vyote (Vya upinzani na CCM).

Nawauliza hivi: Je, mmejipangaje na figusu figisu endapo zitajitokeza katika zoezi zima la uchukuaji, ujazaji na urejeshaji wa fomu za kugombea? Binafsi, naona hili ndilo zoezi gumu zaidi ya kupiga kura. Mgombea unaweza kujiandaa lakini ukaondolewa kwenye mchakato, na mwenzako akapita bila kupingwa, kutokana na au uzembe wako wa kujaza fomu au kufanyiwa figisu figisu na wasimamizi wa uchaguzi.

Wote humu ni mashahidi. Mwaka jana katika uchaguzi wa serikali za mitaa, tulijionea na kusikia figisu figisu zilizojitokeza. Mfano: Msimamizi wa uchaguzi kufunga na kutoonekana ofisini muda wa kazi, na wagombea kuondolewa kwa sababu ya kukosea herufi za majina.

Niwapongeze CCM kwani huwa wapo makini sana katika zoezi zima la uchaguzi, kwa kuzimudu figisu figisu za uchaguzi. Mwaka jana, kiongozi wao, kama sikosei alikuwa Mr Slow Slow alisema wao waliwatafuta wanasheria, ambao waliwasaidia wagombea wao kujaza fomu kwa usahihi.

Kwahiyo, pamoja na kujiandaa na uchaguzi, wagombea wote (Upinzani na CCM) msisahau kujiandaa vyema katika kuchukua, kujaza na kurejesha fomu. Hili ndilo zoezi muhimu sana la awali katika uchaguzi.

Nilikuwa nawakumbusha tu. Ila kama milikuwa mnakumbuka, basi maandalizi mema ya uchaguzi, tukutane Oktoba.

Chonde chonde, isitokee mwaka huu mgombea akapita bila kupingwa kwa sababu tu, wagombea wengine wameondolewa kwa kukosea kujaza fomu, hiyo ni aibu.

Wagombea kabeni mpaka kivuli.
 
Inashangaza sana watanzania wanavyoendekeza ccm kwa zaidi ya miaka 60 sasa. Tunajenga udikteta wenyewe halafu tunaanza kulialia. Wenzetu tunaokwenda kuwaomba fedha kila siku huku Ulaya na Marekani hawakai na chama kimoja zaidi ya miaka 4 au 8 wanabadilisha. Tunapenda fedha zao lakini hatupendi demokrasia yao, haya.
 
Kama ccm inakubarika watoe equal political ground , sio kuleta figusi Juma Maharage jaribu kujitafakari sana unalitia Aibu taifa.
 
Back
Top Bottom