Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Wasalaam wana JF,
Niende moja kwa moja kwenye mada, suala la walimu kama wametengwa ni jambo la kusikitisha sana. Bahati mbaya watu wameamua kwa makusudi kuwakejeli na kuwaona ni daraja la mwisho katika utumishi wa umma.
Kwa wale waliosoma shule miaka ya 2000 kurudi nyuma tunaelewa, walimu walikuwa na hadhi kubwa sana hata kuheshimika na jamii. Kinachoendelea sasa ni ulimbukeni kuona kama walimu ni watu wa chini kabisa.
Inapotokea mwalimu kamjeruhi mwanafunzi kwa bahati mbaya wakati wa kumpa adhabu basi utaona nyuzi kibao kwa unafiki wakimshambulia mwalimu, tukienda mbali zaidi kunaibuka mpaka wasanii huko mitandaoni kushambulia watu eti wameguswa? Punguzeni unafiki kujiona mna uchungu sana wa watoto mambo mengi yanatokea kwa bahati mbaya, baadhi ya watoto wenu ni viburi hata huko majumbani mnawapiga.
Tuacheni unafiki walimu wanapata madhila ya kutopanda madaraja, mishahara midogo, mazingira magumu ya kazi ila ni nan anapaza hizo taarifa? Madhila makubwa ya walimu wanajisema wenyewe hakuna sijui Batuli Actress wala steven Nyerere anayewasema .Utawaona mtandaoni kujifanya wameguswa inapotea mwalimu kamchapa mwanafunzi.
Hakuna mwalimu anayemuadhibu mwanafunzi ili ampe majeraha inatokea tu bahati mbaya, kila kazi ina matatizo yake madereva wanapata ajali na kuua abiria kibao ila akifanya mwalimu inakuwa ni mada kila kona.
Pia soma: Mwalimu wa shule ya Sekondari Mwilibona awapiga wanafunzi wake 2 na kuvimba mikono na damu kumwagika kisa wamechelewa kufika shule