Elections 2010 Kuiba kura, kuchakachua matokeo ya uchaguzi ni UHAINI

Elections 2010 Kuiba kura, kuchakachua matokeo ya uchaguzi ni UHAINI

Joined
Jun 13, 2010
Posts
22
Reaction score
1
Kuiba kura, kuchakachua matokeo ya uchaguzi ni kitendo cha uhaini kwani ni sawa na kupindua serikali. Serikali halali inachaguliwa na wananchi halafu vibosile vichache vinakaa na kula njama na kuamua kucheza na hizo namba ili aliyeshindwa aonekane kashinda na aliyeshinda aonekane kashindwa. Hilo ni jaribio la kupindua serikali na likifanikiwa mapinduzi yatakuwa yamefanyika.

Kwa hiyo wizi wa kura na kubadilisha matokeo ya chaguzi za wapiga kura ni kitendo cha uhaini na adhabu yake kwa Tanzania inaanzia kifungo cha muda mrefu hadi kifo. Hadi sasa wamekuwa wakilindwa na washirika wao na wanaofaidika na uhaini huo lakini siku tutakayowapata itabidi wajibu shutuma hizo za uhaini na wakihukumiwa kifo tutawanyonga - hata kama watakuwa wameshakufa.

Oliver Cromwel wa Uingereza alipindua serikali lakini baada yake kufa walipata mwanya wa kumshitaki kwa uhaini na alihukumiwa kunyogwa. Kwa hiyo walifukua mifupa yake na kuinyonga! Kwani kufa ndiyo kukukwepeshe kunyongwa?
 
Back
Top Bottom