Itabidi akumbuke ni nani amempa kutumia simu yake ikiwa na sim card yake au kamchezea akachomoa sim card na kuitumia. Hii ni zaidi ya kuianika password. Au sivyo naungana na watu wanao doubt kuibiwa hela MPESA hivi hivi kirahisi. Alternatively, iwe ni wafanya kazi wa Voda wenyewe kama mitambo inawaruhusu.
Tetesi kama hizi ndizo ziliwafanya vijana wanaotaka kurudia mitihani NECTA mwaka huu kutokubali kutumia MPESA kulipa ada ya kufanya mitihani. Wote walilipia Posta. Vivyo hivyo Bodi ya Mikopo nayo imeweka utaratibu wa vijana kulipa kupitia MPESA, ZAP, au TIGO PESA badala ya vijana kununua card CRDB ilivyokuwa kwa TCU. Wengi wakifikia hatua hiyo wanaingia mitini ingawaje njia hizi pia zinafanya vizuri. Nimeshuhudia MPESA ikifanya vizuri tu kwa Bodi ya Mikopo. Publicity au Uvumishaji mkubwa unahitajika kuwashawishi vijana wazikubali njia hizi. Kazi kwenu HESLB na NECTA
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.