Kuibuka kwa HERBAL CLINICS na changamoto za kiafya kwa watanzania

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,692
Wanajamvi habari za jioni.

Leo ningepeda kujadili juu ya hizi clinics za tiba mbadala ambazo zimeibuka kwa wingi sana hapa Tanzania na ambazo kiukweli zinaleta changamoto kali sana kwa mamlaka za udhibiti wa tiba na madawa na hata kwa walaji wenyewe.

Sikuhizi karibu kila redio station utaskia wakitangaza juu ya clinics za tiba mbadala na hizi utaskia mara zote wakitaja magonjwa yafuatayo kwamba wanayatibu:-
  • kisukari (diabetes)
  • Presha aina zote
  • prostate
  • kansa
  • HIV
  • hedhi
  • nguvu za kiume
  • chango
  • uzazi nk

Binafsi huwa ni mfuatiliaji zaid wa mada ambazo wenye hizi clinics huzitoa ama kwa njia ya redio ama vipeperushi ama vipindi vya TV.

Jambo kubwa ambalo nimegundua ni kwamba wengi ama wote hawa naweza kusema hawana elimu ya TIBA ama utengenezaji wa dawa, ingawa wanaweza kuwa wanajua elimu ya viumbe hai. Nasema hivi kwasababu sijawah kuona popote pale duniani dawa ikatolewa bila kuonyesha active ingrediaents kwenye dawa husika na contraindications achilia mbali mambo mengine kama pharmacokinetics etc.

Pia sijawah kuona duniani dawa inatengenzwa bila kufanyiwa clinical trial, sisemei convetional medicine bali hata hizi ambazo ni za kienyeji. Mfano mzuri nchini India wanatumia sana dawa za miti shamba lkn hupita kwenye clinical trials kama zilivyo convetional medicines na hizi hukuta zina maelezo muhimu juu ya dawa husika.

Haya basi tu assume hayo yote hatuyapi vipaumbele na tukasema kwakua imemtibu gfsonwin basi na mwingine mgojwa anywe swali kwangu linabaki nani ajuaye fate yake?? je wagonjwa wanaozitumia huwa wanafanya Blood Biochemistry kujua hatma ya hizi dawa?? ama kisa imenitibu presha hata kama ikiua maini ni sawa??

hilo ni dogo manake hakunaga mtu aliyewah kufa akasifiwa marehem kaenda na viungo vyake vyote vikiwa vizima, kubwa kuliko yote unakuta mtu ana justfy kutibu magonjwa hadi 40 lkn ukichunguza mti ni huo huo ila akapaki vichupa tofauti tofauti sasa huu sio wizi?? si bora apaki kwenye kifungashio kimoja ila aonyeshe kwamba unatibu magonjwa yote haya??

Kana kwamba haitoshi watu hawa hutoa elimu za uongo juu ya afya, na inaumiza sana pale mtu anapoongelea maswala ya afya halafu anamislead watu. tena ili kujizidishia wateja anaacha kabisa kuongea habari za lishe bora, na usafi anakazania kuhubiri products zake zinavyotengeneza afya ya mgonjwa hata nje ya lishe bora hivi kweli huu si uuaji??

Jamani wanajamvi wenzangu tiba bora unaweza kuipata Hospitali pekee kwa watu ambao wako trained na kila siku wanaongezewa maarifa. Afya yako mgonjwa utaiboresha kwa kula chakula bora, kumeza dawa sahihi, na kuwa msafi basi nje ya hapo ni uongo tu. Kumbukeni kwamba kwa kula mlo kamili unapata virutubisho muhimu kwa ajili ya kupambana na magonjwa, kukuza mwili, kutia nguvu na joto na hata kuimarisha mifupa na kungeza damu, na kwa kuwa msafi unajikinga na magonjwa hasa yaenezwayo kwa iyo lishe bora na usafi ni muhimu kuliko hata hizo dawa zinazotangazwa na hawa wachumia tumbo.

NAOMBA IELEWEKE SINA NIA YA KUHARIBU BIASHARA YA MTU, BALI NINASEMA KWELI MANAKE WAMEZIDI KUTUIBIA MTU JUZI ULIKUWA UNAHUBIRI HABARI ZA MAFREE MASON LEO NAWEWE NI DR UNATIBU KWA MITISHAMBA HUU NI WIZI MTUPU.

Nawasilisha
 
vipimo vyenyewe unawekwa mbele ya computer anaclick click ......mimi na ujanja wangu nilipimwa na computer eti...wana sound hao ....duuuh
 
haswa wakenya ndo wengi sana kwenye hii issue...me naona ni wizi tu hakuna lolote...
 
mbaya zaid hata principles underlying matibabu hawazijui.

unakuta anakwambia HIV ni ugonjwa kwa unayejua unabaki heeh!!
 
haswa wakenya ndo wengi sana kwenye hii issue...me naona ni wizi tu hakuna lolote...

kuna siku nilikuwa natokea nairobi ...akapanda kwenye bus mkenya mmoja ...aisee anavohubiria hiyo dawa loh...kama ni mgonjwa unaona umeshapona hata kabla ya kutumia...that guys ni something else kwenye kusoundisha bana loh
 
haswa wakenya ndo wengi sana kwenye hii issue...me naona ni wizi tu hakuna lolote...

ni kweli kabisa na si unajua wakenya wengi ni watu wa kazi za kiutapeli tapeli??

Hapa ubungo stendi kuna mkenya mmoja alikuwa na hubiri mambo ya free mason kila siku toka mwaka 2010 ndo nilianza kumwona cha ajabu leo nimepita hapo nimemkuta nae ana uza dawa eti anatibu na anajiita Dr nikajiuliza hivi jamani watu wanacheza na maisha enh??
 
kuna siku nilikuwa natokea nairobi ...akapanda kwenye bus mkenya mmoja ...aisee anavohubiria hiyo dawa loh...kama ni mgonjwa unaona umeshapona hata kabla ya kutumia...that guys ni something else kwenye kusoundisha bana loh

umenichekesha sana.
ukweli ni kwamba hizi dawa sio kweli kwamba zinatibu na kama zinatibu basi madhara yake ya mbeken hayajulikan lkn wao wana uwezo wa kumshawishi mtu na akaamini kwamba zinatibu na ni nzuri kabisa
 
vipimo vyenyewe unawekwa mbele ya computer anaclick click ......mimi na ujanja wangu nilipimwa na computer eti...wana sound hao ....duuuh

kuekwa kwenye computer ile ni program tu ambayo itadefine kulingana na info zilizokuwa fed in. hivyo usije ukaamini kabisa hizi tiba.

vipimo vya kutumia kwenye computa kama vile biosensors ni very expensive walalahoi hawa hawawez kuafford kununua
 
kazi ni pale unapomwambia doz inachukua mda gan anasema we kunywa tu ukiona maumivu yameisha acha. na maajabu mengine vpimo ndo wako ovyo waulize dawa ya maji na takiwa ninywe ml ngap akikujibu jiite unabahat sana
 
umenichekesha sana.
ukweli ni kwamba hizi dawa sio kweli kwamba zinatibu na kama zinatibu basi madhara yake ya mbeken hayajulikan lkn wao wana uwezo wa kumshawishi mtu na akaamini kwamba zinatibu na ni nzuri kabisa
yaani kama una hela unaweza ukanunua mzigo wote!la all in all serikali yetu haijali kamwe! hadi wachina wanaingiza madawa yao huku feki ...wamasai nao yaani hii miili hii
 
Lakini mkuu hii kitu ya tiba asili sio Tanzania tu ni dunia nzima..Na ilianza USA baada ya serikali yao kukuta wanatumia more than $1 trillion(dola trillion moja) kwenye mambo ya afya tu kwa mwaka, na katika kupunguza hili wakaja na suala zima la tiba mbadala...

Kimsingi tiba mbadala sio mbaya ila wafanya biashara wa kibongo ndio wanaoiharibu dhana hii kwa ujumla, kwani mataifa yoote duniani yamegundua kuwa inawezekana kupunguza bajeti za afya kwa kurudi katika asili na hasa vyakula na herbs..

Na wameweza sana, juzi nilikuwa nasoma classified document(reserach) fulani ya matibabu ya kansa kutoka marekani, inadai kuwa makampuni ya kutengeneza dawa za kansa hasa level one na two yamekuwa yakitumia matunda ya stafeli kutengeneza dawa zao na ili kukwepa kupunguza faida inayotokana na biashara ya dawa hizo wakaamua kuficha kuwa dawa hizo zinatengenezwa kwa 100% na mmea huo wakadai kuwa serikali kwa kuwa wametumia kiasi kikubwa sana cha fedha katika research hiyo na bado ugunduzi haujarudisha fedha iliyotumika hivyo basi jamii ifichwe mpaka muda muafaka utakapofika, lakini bahati mbaya zikavuja..

Tunaoweza kuwalaumu hapa ni wabongo kuchakachua taaluma hii kwani wao huamini kila kilichotoka kwenye mtandao wa internet ni sahihi, na serikali kutokuwekeza huko pia kwa maana ya vifaa na reseach ili kujua contents za hizo tiba mbadala chemically ni nini..

Ila kwa sasa dunia nzima inahamia katika tiba hizo na ni kitu kisichoweza kuepukika kwani medical science imeanza ku-fail kutoa majawabu kwa baadhi ya matatizo na magonjwa
 
kazi ni pale unapomwambia doz inachukua mda gan anasema we kunywa tu ukiona maumivu yameisha acha. na maajabu mengine vpimo ndo wako ovyo waulize dawa ya maji na takiwa ninywe ml ngap akikujibu jiite unabahat sana
jamani yani haya ni majanga kwa kila mtanzania kwa sasa. kuna mmoja nilimuuliza kwann anasema eti mgonjwa wa ukimwi anywe vijiko vi3 vya mafuta ya ubuyu kila siku akasema eti ili aongeze CD 4 nikamuuliza hivi unajua digestion ya lipids jins inavyotake place?? akawa hajui na je mafuta kama mafuta huingizwa mwilini kupitia nini?? hajui, nikamuuliza kazi ya nyongo kwenye mafuta ni nini?? na penyewe hana jibu nikamwambia wewe unaua wagonjwa na kama mgonjwa wako atarudi kwako baada ya mwaka akiwa hai basi utakuwa una bahati......
 
...nice explanation mkuu...sio kwamba tiba asilia mbaya kwa kweli....kuna mitishamba ni dawa nzuri tu ..ila tatizo ni jinsi jamii ilivolichukulia hili swala...yaani watu wametake easy kwa asilimia kubwa imekuwa ni maficho ya utapeli....mtu anachanganya tangawizi na iliki as long anajua haitokudhuru anakwambia inatibu kitu flani tumia miezi fulani kunywa na supu nzito...si unajua hii miti shamba inapenda supu hiyooo! haitumii maji....
 
asigwa sipingani na wewe kabisa na wala siipingi tiba asili hata kidogo ninacho kipinga mm ni kwamba hwa wenzetu wamezidi usanii na hawana elimu juu ya wanachokifanya na hivyo kuzidi kuyaweka maisha at risk.

Mfano NIMR wana kitengo cha tiba mbadala na hata MUHAS wanacho hawa dawa zao hupita kwenye taratibu za kawaida za kitaalam za kugundua dawa na ukweli wana dawa nzuri sana. na hata waganga wengi wa tiba asili huwaona hawa watu wakajadili nao na kama ni dawa mganga anayo basi hufanyiwa tafiti na ikionekana kweli inatibu basi dawa hii huchukuliwa na kuanza field trial.

niseme tu mahali kama NIMR wamekuwa wakitafiti dawa hizi na nyingine tayari ziko sokoni ingawa production bado iko chini, lkn za hawa wanao hubiri huko njian utashangaa dawa hata composition haina.
 
Last edited by a moderator:
hayo mafuta ya ubuyu usinikumbushe nilimnunulia baba yangu aisee eti yanaponyesha sukari...ila ni mazuri sana kupaka vipapatio!
 
swala hapa ni je kweli kilichoambiwa kiko ndani ya dawa husika kweli kinatibu?? na je huyu mtoaji dawa amewah kufanya majaribio wapi?? Smile kuna cases mfano alovera wengi wanasema ni dawa sawa lkn hakuna anayejua active ingredient kwake ni ipi na itumike kwa kiasi gani, kuna cases za watu wameji overdose na mualovera na hivyo kuua mafigo na maini kabisa.

hata mwarobaini ni hivyo hivyo, swala si kuwa na medicinal properties swala ni je active ingredient kwake ni ipi?? na je haina complication kiasi cha kuhitaj synthetic form??

kwa case ya mwarobaini ni sumu kabisaa lkn active ingredient yake ambao ni quinine inatibu malaria kinachofanyika huwa wanachukua synthetic form basi ile ambayo ni sumu inabaki sasa ukija kwa hawa waganga wetu wao wanakupa yote pasi kujali haya.
 
Last edited by a moderator:
hayo mafuta ya ubuyu usinikumbushe nilimnunulia baba yangu aisee eti yanaponyesha sukari...ila ni mazuri sana kupaka vipapatio!

mafuta ya ubuyu kama yalivyo mafuta mengine process ya digestion kwake ni ngumu hata ukinywa mafuta ya alizeti leo hutaskia njaa mapema manake process ya emulsification kwake ni ngumu na isitoshe inahitaj nguvu but huzalisha nguvu zaid baada ya kuvunjwa vunjwa hii dio underlying concept but watu wanadanganywa weee utafikiri sijui ni kitu kipya.
 
Ha ha ha nimeipenda hii ya supu(mchemsho)

Ni kweli Tanzania hatuna vyombo vya utafiti na hili ndilo tatizo, juzi nimepita pale ferry jamaa mmoja alikua anaelezea madhara ya kaloraiti wanayopaka kina mama usoni pamoja na griseline nikashangaa sana.

Jamaa kawakusanya watu kama mia kadhaa hivi wasiojua mambo ya chemistry wala chemical reactions, kachukua gazeti kalipaka calorite halafu juu yake kamwaga griceline kidogo halafu kachukua ile GV ya kusafishia vidonda alipoimwaga tu gazeti liawaka moto likateketea loote, watu wakabaki modomo wazi , Wakashindwa kuelewa ni kwa temperature gani hiyo chemical reaction na kwa level gani ya humidity na mgandamizo(atmospheric pressure) hayo hutokea.

Nilipomuuliza kuwa kwa kuwa unaamini kuwa maji yanachemka kwa 100 degree Centigrade je haamini kuwa maji hayo hayo tukiyapa pressure fulani yaweza kuchemka katika 20 dgree Centrigrade vile vile, akasema yeye hayo hayajui na hajui lolote kuhusu chemistry na shule hajakanyaga..Nilipomuuliza kuhusu contents za hivyo alivyochanganya vikatoa moto ni zipi hakujua vile vile.

Lakini cha ajabu ana majarida na ana vibali vyoote vya afya kuwa ni "certified professional"..hapa ndipo nikajua kuwa tatizo ni elimu tu hakuna jingine...

Japo hawa jamaa wanafanya kazi ya maana na wana facts ambazo kama hujapita level zile huwezi kuwabishia, lakini wanasaidia mengi na wanasaidia wengi vile vile
 
Nimekuelewa sana mkuu, na mimi kinachonitatiza ni vibali na vyeti vya uthibitisho walivyo navyo hawa watu kwani inaonesha wana vibali vyoote kutoka wizarani na hata Muhimbili kufanya shughuli zao, japo hata madawa waliyo nayo hawayajui yanaundwa na nini

Kwa kuwa inaonekana wanawasaidia watu japo kwa trial and error nadhani imefika wakati serikali ianzishe kabisa chuo cha tiba mbadala na wapewe elimu yao bila urasimu kwani hata hizo tafiti za NIMR ni gharama sana kuzifanyia kazi na dawa zao japo zinatumia hii hii mimea inayouzwa shillingi mia sokoni wao wanauza madawa kwa malaki sasa kwa nini watoto wa mjini wasi-take advantege hapo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…