Abdalah Abdulrahman
JF-Expert Member
- Aug 29, 2019
- 222
- 202
Idadi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii Tanzania imeongezeka kwa kasi na kufikia 4.5 Milioni. Idadi hii imegawanyika katika makundi makubwa mawili,Kundi la kwanza ni wale wanaotumia mitandao ya kijamii kwa manufaa bila kuvunja Sheria,na Kundi la pili ni wale wanaotumia mitandao ya kijamii kwa uhalifu. Idadi ya wanaotumia mitandao ya kijamii kufanya uhalifu ni ndogo ukilinganisha na idadi kubwa ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa manufaa.
Mitandao ya kijamii kama Jamii Forums, Facebook, Twitter, Instagram, imekua ikiwanufaisha wafanyabiashara,wanasiasa,wakulima na wafanyakazi.Mitandao hiyo hiyo imekua ikitumika na wahalifu kufanya wizi wa fedha,kutukana viongozi,kudhalilisha watu pamoja na kutekeleza jinai zingine.
Tatizo katika mitandao ya kijamii linatokana na uhuru usio na kikwazo ambao unaweza kusababisha madhara makubwa ndani ya jamii.Udhibiti wa mitandao ambayo inatoka nchi zingine ni mgumu kutokana na sheria za zinazolinda ule mtandao wa kijamii.Mfano si kushabikia mapenzi ya jinsia moja kwa mitandao kama Facebook,Twitter,Instagram na WhatsApp,kinyume chake ni kuwa mitandao hii inajali Kundi la watu hawa na inawapa kipaumbele maalumu.
Mifano hii na mingine inaweza kuleta madhara ndani ya nchi kama vile kupenyeza chuki za dini,rangi na ukabila ndani ya jamii.
Zipo nchi kama China,Urusi na zingine ambazo hazitumii mitandao hii ya kijamii kutokana na madhara yanayoweza kupatikana kutokana na matumizi ya mitandao hii.Badala yake imeanzisha mitandao yake ya kijamii na imekua inafaida kubwa kwa nchi na usalama wa nchi.
Nitatoa mifano ya nchi za Afrika ambazo zimewahi kupata hasara kubwa kwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
1. Misri
Ndani ya nchi ya Misri waandamanaji wachache waliweza kutumia mitandao ya kijamii kupotosha umma na kufanikiwa kuandaa maandamano January 25, 2011 ambayo yalisababisha mapinduzi
2. Tunisia,
Tunisia kama nchi zingine za Afrika ina changamoto ya ajira,changamoto hii ilitumika na wapinzani wa serikali.Kijana mmoja aliamua kujichoma moto kwa kupinga ukosefu wa ajira na kusambaza video hii kwenye mitandao ya kijamii.Watu waliandamana katika miji ya Sfax and Tunis kwa kujiweka pamoja kwa njia ya mitandao ya kijamii. Rais Ben Ali alikimbia na kuacha nchi ikiwa na maandamano yaliyosababisha vifo na hasara kubwa.
3. Kenya
Hali ya Kenya mwaka 2013 inaonesha kuwa wanasiasa walitumia mitandao ya kijamii kwenye kampeni zao.Kampeni hizi ziliibua hisia za ubaguzi na mambo mengine ambayo yalisababisha fujo zilizoua Wakenya wengi.
Hivyo basi uhuru wa mitandao ya kijamii unapaswa kupimwa madhara na faida zake hasa kipindi ambacho ni muhimu kama kipindi cha Uchaguzi. Pia serikali iweke utaratibu wa kuhamishia Wananchi katika mitandao ya kijamii ambayo imesajiliwa nchini kama Jamii Forums ili kudhibiti maudhui.