Richard Baziwe
Member
- May 16, 2017
- 6
- 5
Leo nimeona ni vyema niwaletee uzi huu hasa kwa wakulima wadogowadogo wa mikoa yote Tanzania.
Lengo ni kuonesha changamoto zilipo kwenye sekta hii. Mifano yangu mingi itagusa mikoa ya kanda ya kati hasa Singida na Dodoma maana ni miongoni mwa mikoa ambayo wakati mwingine ukumbwa na njaa katika baadhi ya wilaya zake japokuwa watu wengi watakwambia ni kwa sababu ya ukame kanda ya kati lakini kwa mtazamo mwingine ukame ni ziada tu.
Kumekuwa na changamoto sana ya kipato kwa wakulima wadogowadogo wa mikoa mingi Tanzania mbali na kauli mbiu ya "kilimo ni mgongo wa taifa" na nyingine mbalimbali kutoka kwa viongozi wa serikali.
Tumeamini katika hili na ni kweli kama kilimo kingekuwa chenye tija wakulima wengi tusingekuwa tunaishi kwenye mazingira magumu sana maana kilimo ni ajira nzuri sana.
Ni changamoto nyingi zinazowakuta wakulima maana siku msimu ukienda vizuri kwa wakulima, soko linakuwa vibaya kwa wakulima na siku soko likiwa vizuri ndio msimu unakuwa mbaya kwa wakulima.
Kwa miaka mingi yamekuwepo matamko mengi kuhusu sekta ya kilimo hivyo kama matamko yangekuwa yanatiliwa maanani tusingekuwa tunawaona wakulima wakiwa na hali ngumu au kusikia njaa mkoa au wilaya fulani.
Kwa wakulima wa kanda ya kati hasa kwa mikoa ya Singida na Dodoma, kilimo chao kikubwa ni Alzeti, vitunguu, uwele, mahindi, choroko, mtama, viazi vitamu na zabibu kwa maeneo machache ya Dodoma.
Kwa wakulima wa mikoa hii kumekuwepo shida sana kwenye kilimo mbali na ukame kama nilivyotangulia kusema mwanzo.
Changamoto hizi zinaweza kutatulika lakini bado zinaonekana ni ngumu kwasababu serikali inayolenga kuinua uchumi na kipato cha mwananchi bado kwa mkulima au katika kilimo nguvu ya kuleta mapinduzi haijawekwa. Katika hili nitazungumzia mambo machache kama ifuatavyo:-
1. Ugawaji wa mbolea ya ruzuku katika maeneo machache.
Kwa kilimo chenye tija ambacho tunakiita kilimo cha kisasa tunachotegemea kimuinue mtanzania wa hali ya chini kumleta kwenye uchumi wa kati, ni jambo la kushangaza kwamba mkulima analima na kupanda mpaka kuvuna bila kutumia mbolea.
Nakubali kwamba kuna baadhi ya maeneo bado yana rutuba ya asili na wakulima wengine wanatumia samadi na mboji lakini kwa maeneo makubwa ambayo yametumika kwa shughuli za kilimo kwa muda mrefu ni jambo la wazi kuwa yahitaji mbolea ila angalau kwenye tathmini tuseme mkulima anavuna labda kuanzia gunia 10 hadi 15 kwa hekari ya mahindi japo na penyewe ni kwa kadirio la chini maana hekari inatakiwa kuanzia gunia 20 na kuendelea kama ni mahindi.
Kwa maeneo ya kanda ya ziwa na nyanda nyinginine ambazo ni mvua ni nyingi na majani yapo ni rahisi kutengeneza mboji. Ila mboji si rahisi kwa maeneo mengi ya kanda ya kati kwani wakati wa kiangazi majani karibia yote hukauka na kuliwa na mifugo na mabaki hupeperushwa na upepo hivyo mashamba yaliyo mengi hubakiza udongo tu kiangazi chote kwahiyo ni vigumu kutengeneza mboji. Na kwa wachache wenye mifugo ndio hutumia samadi katika mashamba machache kwani si rahisi kwa mtu mwenye kulima hekari tano kuwa na samadi ya kutosheleza eneo lote. Mbolea ya ruzuku imekuwa ikitolewa kwa wilaya chache ukilinganisha na uhitaji wa wakulima kimkoa, na mara nyingi hii mbolea ya ruzuku hawapewi wakulima wa kanda ya kati bali inapelekwa mikoa ya kusini na baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa hasa Geita na Mwanza. Hivyo wakulima wa kanda ya kati mara nyingi hawapati mbolea ya ruzuku.
Na ardhi ya mikoa hii ni ardhi inayohitaji mbolea kila mwaka na inatakiwa mbolea kupatikana mapema maana mvua ni za muda mfupi. Lakini jambo hili limekuwa tatizo hivyo mwisho wa siku huwalazimu wakulima kupanda bila mbolea na kukuta mtu anaambulia gunia 4 au 6 kwa za mahindi kwenye hekari nzima. Kutokana na mikoa hii kuwa na tatizo la kiasili yaani uhaba wa mvua, kwani maranyingi wakulima wa kanda ya kati wana msimu mmoja wa mvua, yaani za masika ambazo maranyingi huanza mwezi Novemba mwishoni au Disemba mwanzoni na ni za mkulima kukimbizana nazo maana akichelewa kidogo halimi tena kwani masika ya mikoa hii hukatika mapema na hivyo maranyingi mazao kukaukia shambani kabla ya kukomaa na hivyo kupelekea mavuno haba na njaa.
Hivyo wanastahili mbolea mapema na kulima kwabla ya mvua kuanza ili zinapoanza wanapanda.
2. Pembejeo nyingine za kilimo kama mbegu na viuatilifu kuwa ghali sana.
Mara nyingi pembejeo za kilimo zimekuwa ghali sana kwa mikoa hii. Mbegu za kisasa zinazoshauliwa kilimwa ili kuongea mazao ni ghali sana. Kwa mfano, mwaka jana mfuko wa mbegu ya mahindi ya kisasa kilo mbili ilienda mpaka Tsh 15000/- na nyingine Tsh 18500/- naomba nisitaje majina ya makampuni. Vivyo hivyo katika mbegu za alzeti ambayo mfuko wa kilo mbili mbegu ya kisasa ni elfu 14,000/-.
kwa mtazamo wa kawaida unaweza kudharau lakini hizi gharama si kitu chepesi kwa mtu wa hali ya chini. Hivyo hii hupelekea wakulima kurudiarudia mbegu za asili na kupunguza tija katika mavuno.
Serikali ikifanya utaratibu mzuri kwenye kupunguza bei ya pembejeo ni wazi kwamba wakulima wengi watanunua na kupanda mbegu zenye tija na kupata mavuno mazuri.
3. Kukosekana kwa Miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika mikoa hii hakuna kabisa, hivyo mvua zisipokuwa za uhakika hakuna njia mbadala ya wakulima kunywesha mazao yao shambani zaidi ya kuyaacha yakauke na msimu huo kuishia kwenye vilio.
Soko pia limekuwa shida kwa kidogo tu kinachopatikana. Hii ni karibia kwa mikoa yote kwani miundombinu ya ununuzi wa mazao bado ni shida sana. Kwa mfano miaka kama minne iliopita wakulima wengi wa Singida walijikita katika uzalishaji wa viazi vitamu na choroko.
Kwa kipindi hicho lilikuwepo soko kwa wahindi maana ndio walikuwa wanunuzi wakuu wa mazao hayo. Lakini badala ya serikali kuboresha mazingira ya wanunuzi hawa, yenyewe ilizuia kuuzwa mazao nje hivyo kusababisha wakulima kuingia hasara kubwa maana gunia la viazi lililokuwa linauzwa Tsh 60000/80000/- lilishuka na kuuzwa Tsh 10000/15000/-. Choroko ilikuw Tsh 120000/- ilishuka na kuuzwa Tsh 60000/-.
Kwa hali kama hii ni ngumu mkulima kuinuka kiuchumi.
Kwa maelezo hayo naomba niishauri serikali kufanya mambo yafuatayo ili kumuinua mkulima wa kila mkoa ukizingatia kwamba ajira kuu iliobaki kwa vijana na wazee, kwa wasomi na wasio wasomi ni kilimo. Nasema niishauri serikali kwasababu ikiweka mazingira mazuri ya watu kujiajiri katika sekta ya kilimo itapunguza sana tatizo la watu kutokuwa na ajira.
Vilevile ni sehemu ya kupatia ushuru wa namna mbalimbali na kuongeza mapato ya nchi. Mambo haya ni yafuatayo:-
1. Kuhakikisha serikali inakuwa na asasi zake za kuchunguza tabia ya chi ya maeneo fulani au kanda na kuzalisha zinazoweza kustahimila hali ya maeneo husika kwa mfano maeneo kama ya kanda ya kati yanahitaji mbegu za muda mfupi, vilevile wazalishe mbegu za gharama nafuu ili kumraisishia mkulima wa hali ya chini kumudu kununua hizo mbegu bora.
Wanapoachiwa makampuni binafsi kwenye suala la utafiti wa mbegu, mbali na kwamba ni suala linalohitaji gharama lakini mara nyingi watalenga kujipatia faida kubwa na ndio maana mbegu zinauzwa ghali.
2. Kusambaza mbolea ya ruzuku mikoa yote.
Usambazaji wa mbolea uwe ni wa aina zote yaana ya kupandia na kukuzia na sio aina moja tu maana maranyingi utakuta watu wa eneo fulani wanajua urea tu kwamba ndo mbolea.
Ile kasumba ya kupeleka mbolea ya ruzuku kwenye mikoa fulani au wilaya fulani kwakuwa zimezoeleka zinazalisha sana ifutwe maana maeneo mengi ya nchi yetu bado yanaweza kuajiri watu wengi katika kilimo. Vilevile upatikanaji wa viuatilifu uwe rahisi kila sehemu na kwa gharama nafuu ambayo watamudu wakulima wa jembe la mkono.
3. Ubora wa soko.
Mbali na kwamba mkulima anatakiwa atafute soko la mazao yake, lakini pale mazao yanapokuwa yamezalishwa kwa wingi Serikali inatakiwa itafute soko kimataifa na ndio maana sisi na nchi nyingine za Afrika tumepata shida ya ngano baada vita ya Ukraine na Urusi.
Ni wajibu wa nchi na viongozi kuwatafutia soko wazalishaji na kufungua mipaka kwa nchi jirani hasa kwa wale wanaohitaji mazao ya chakula kama mahindi, mchele mbaazi na maharage na si kuwawekea vikwazo wanunuzi wa nje wakati mazao kwenye soko la ndani yanadorora. Hii itasaidia mkulima kupata kipato kikubwa na serikali kujipatia fedha za kigeni.
4. Utengenezaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.
Mbali na kwamba maeneo ya kanda ya kati yana uhaba wa mvua lakini haimaanishi kwamba njia za maji za ardhini hazipo.
Hivyo kuna uwezekano wa kuchimba visima vya chini na kupata maji mengi sana kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Kwa hali ya kawaida ukifikiria unaweza kuona ni gharama kubwa.
Lakini unapojenga miradi kama hii ni ya kudumu kiasi kwamba hata wakulima wakuambiwa kuchangia ni rahisi maana wataona manufaa yake.
Iwapo mazingira ya namna hiyo yatakuwepo kwenye kilimo nadhani ni rahisi kwa watu wote hasa vijana na hata wasomi wasiokuwa na ajira kujiwekeza kwa bidii katika kilimo kama ndio sehemu ya ajira yao ya kudumu. Hivyo tatizo la ajira litapungua kwa kiasi kikubwa hata kama halitoisha kwa sababu ya wachache wasiopenda shughuli za kilimo na wale wanaopenda kukaa mjini tu hata kama hana chochote cha kufanya kwa kutopenda kuishi kijijini.
Na hii si kwa mikoa ya kanda ya kati tu bali karibia mikoa yote au wilaya nyingi zenye wakulima zinafanana katika changamoto hivyo kuzidi kuwajengea baadhi ya watu fikra ya kilimo kuonekana kama si ajira na ni kazi ngumu.
Wengine wanadhani ni kazi ya watu ambao hawajasoma lakini tunatakiwa tujue kuwa hata mapinduzi ya viwanda huko kwa wenzetu mfano, Marekani yalitokana na kilimo. Hivyo hatuna budi kuwekeza vya kutosha katika kilimo.
Nawakaribisha..

Upvote
2