SoC02 Kuishi kwa malengo na maisha ya vijana

SoC02 Kuishi kwa malengo na maisha ya vijana

Stories of Change - 2022 Competition

Alfa king jr

New Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
3
Reaction score
3
KUISHI KWA MALENGO NA MAISHA YA VIJANA.

Malengo na ngazi muhimu katika kufikia mafanikio. Hali ya kuishi ukiwa na matarajio maalum ambayo ambao ungependa utafikiri katika maisha yako kwa hapo badae. Kuishi kwa malengo ni jambo muhimu katika maisha ya vijana mwenye maono ya kufika mbalimbali kwenye maisha. Hii pia itamjenga kijana kuacha kuishi kwa mazoea, kutambua thamani yake na njia za kufikia malengo aliyojiwekea mwenyewe katika maisha.

MAONO. Hii ni picha halisi ya wapi kijana anatamani kufikia katika maisha yake. Maono pia humpa kijana mwongozo wa wapi anatakiwa kupafikia na pia kuweka mikakati halisi ya namna ya namna ya kuyafikia hayo maono. Ukiwa kijana mwenye maono ya kufanikiwa katika kile anachokifanya iwe biashara, masomo na mengineyo, ni lazima utaweka utaweka malengo yako ili uweze kufika ndoto yako. Kumbuka ukiishi kwa malengo utafika kilele cha mafanikio yako na kamwe haitapoteza njia. Maisha ni safari kwa hiyo kujua unaoelekea ni muhimu kabla haujaanza kupiga hatua. Ni vizuri tujue wapi tunataka kwenda kabla ya kuanza safari ili tufike mahali sahihi.

kuishi kwa malengo ni kuweka msukumo katika maisha yako wa mahali unapotaka kupafikia katika maisha yako. Ingawa kuwa na maono na na kuweka malengo ni hatua ya kwanza tu katika kufikia mafanikio. Ukiacha kujiwekea malengo yako ni muhimu kuanza kuchukua hatua kuelekea kutimiza ndoto zako. Kua na ndoto katika akili zetu haitoshi tu bila kuyaishi hayo malengo ni kuchukua sura ya vitendo zaidi.

Vijana wengi wanaishi bila maono wala malengo kwenye maisha hali inayopelekea kuona kila wanachokipata ndiyo sitahiki zao, na wengine wanakata na kukatishwa tamaa kiurahisi kwa sababu wamekosa msukumo wa ndani katika kufikia malengo yao. Ukienda bila maono ni dhahiri itakosa mwongozo sahihi na kila itakapofikia patakuwa halali kwako kwa kua hukupanga kufika popote. Unaishi bila malengo kama mnyama ambaye hujali tu kula, kulala na kuamka na maisha yaendelee.

Kuna faida nyingi za kuishi kwa malengo na kuwa na maono katika maisha . Hizi ni baadhi ya faida;

Maono na malengo hatamsaidia kijana kujitambua. Kijana mwenye maono siku zote anajitambua na kutambua dhumuni la maisha yake, kwa sababu anajua ni wapi anaelekea na badae atakuwa wapi katika sikua za usoni hivi kuweka vipaumbele na mikakati ambayo itaifuata ili kumfikisha moja kwa moja kwenye mengi yake.

Kujua wapi unaelekea na nin ukifanye ili kufika pale huzalisha kujiamini katika kupambana na kufikia malengo na kuwekeza muda wako mwingi katika kudili na mambo binafsi yenye maslahi katika kufika ndoto zako na siku kupoteza muda kwenye malumbano na mijadala isiyo na msingi katika taswira ya maisha yako . Maneno yatamfanya kijan kutazama mbele na kuacha na yaliyo pita kufanya tathmini na kujiendeleza zaidi kwa ujasiri mkubwa.

Maono pia humwongezea kijana msukumo wa ndani kufikia malengo; siku zote safari ya mafanikio ni ngumu na ina vikwazo vingi mara nyingi vijana waliokosa maono ni rahisi kukata tamaa, kulaumu, kulumbana,bila sababu za msingi na kujiona wanyonge. Lakini vijana wenye malengo mara nyingi mawazo yao yatalenga kutimiza ndoto zake na si vinginevyo, kwa sababu sababu hawatatazama ugumu wanaokutana nao bali watalenga zaidi wapi wanataka kufika pamoja na changamoto nyingi watakazozikabili maono yao yatayeyusha vikwazo vyote kwa sababu watakua wamedhamiria kufika kwenye lengo. Usipokuwa unakoelekea kila njia mbele zako itakua ni halali yako na ukikutana na mbwa mkali utaachwa njia na kushika njia nyingine na nyingine kwa sababu unaenda tu ilimradi hakujua ni ipi njia sahihi kwako unatakiwa kuifuata na kukabiliana na kila kilicho mbele yako kama kizuizi.

Maono kutusaidia kufanya uchaguzi wa kipi tufanye na kipi hatuwezi kufanya. Ukiwa na maono utakua na vipaumbele katika maisha .utajua ni kipi unatakiwa kufanya na kipi hutakiwa kufanya katika safari yako ya kufikia mafanikio. Sio kila kitu utakifanya au utaenda kila sehemu. Malengo yatakuongoza nini ukifanye ili kufikia malengo. Kwa namna hiyo haitapoteza muda katika vitu ambavyo havina mchango wa moja kwa moja kwako katika malengo yako. Haitakua mtu wa kutangatanga bali utakua mtu mwenye kujua nini unakifanya na unafanya kwa ajili gani ili ikisaidiwa nini? Mtu mwenye malengo huishi katika njia sahihi na ni mtu wa kitofauti katika jamii.

Watu wenye malengo hujali muda. Kila dakika, kila lisaa,mwezi na mwaka unapopita wanafanya tathmini ya nini wamekifanya na wameonesha utofauti gani na hapo kabla, nini kiongezeke wapi walikosea na nini kifanyike. Tofauti na mtu asiye na malengo hawezi kujua kama amepiga hatua kiasi gani kwa muda gani na nini afanye, hivyo ataishi kwa mazoea ya siku zote na kujikuta yuko palepale. Mtu akiishi kwa malengo atajali muda na kufanya mambo kwa wakati . Watu wasio na malengo wanakua na muda mwingi wa kupoteza kwa sababu hawana misukumo yoyote ndani yao. Mwenye malengo utaletwa nini ufanye na kwa wakati gani na kuchukua hatua za makusudi ili kupiga hatua bila kusubiri kesho.

Kuchagua watu sahihi, upande sahihi, na kundi sahihi kwako kutimiza ndoto zako. Mtu mwenye malengo atahakikisha kwamba kila mtu amekuja kwenye maisha yake anaongeza kitu katika safari yake ya mafanikio na si kuruhusu watu kwenye maisha yao wasio sahihi na wenye kuwapotezea muda .Usiruhusu kuchangamana na watu, makundi,au jamii,ambayo itakupotezea muda na kukuchelewesha katika kufikia malengo. Sio kila watu wanafaa kuwapa nafasi katika maisha yako.ukiishi kwa malengo utakua na marafiki sahihi wenye mchango katika kutufikisha katika sehemu sahihi.

Kuishi kwa malengo huleta nidhamu katika maisha. Ili ufanikiwe katika maisha unatakiwa uwe na nidhamu katika namna ya kuishi kwa usahihi kwa kufuata njia sahihi ikiwepo matumizi sahihi ya rasilimali na muda. Maono na malengo huwa havikupi uhuru wa kuishi na kufanya mambo ovyo bali kumfunga mlengwa katika njia na matendo sahihi ili kufikia malengo. Ndiyo maana watu wasio na malengo huishi wanavyotaka na kufanya kile wanachojisikia hawawezi kuchuja ,kujitoa au kutawala matendo vyao kwa sababu hawana mwelekeo wowote kwenye maisha .

Ni juu wito kwa vijana kuacha kuishi kwa mazoea . Maisha ya kuishi bila maono mwisho wake huwa haueleweki pia. Weka malengo, anza sasa kutimiza ndoto, muda na wakati sahihi ni sasa kutengeneza maisha yako ya badae.

Alfa king jr.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom