Kuishi pamoja!

Kila mtu aishi maisha yake na afanye maamuzi kutokana na kile anachoona sahihi kwenye maisha yake....kwangu mimi sidhani kama ni kujidanganya mtu kuona watu wanaoishi pamoja kabla ya ndoa kama wanakosea....katika kila kitu binadamu tunaongozwa na misingi fulani kama dini,elimu,tamaduni...na si lazima tuwe perfect kwenye hiyo misingi ndo uunge/kutounga mkono hoja fulani fulani....

Hakuna ndoa iliyo perfect,wala haitakaa iwepo....haijalishi mliishi pamoja mkajuana sana kabla ya ndoa au hamkuishi,changamoto ziko pale pale...vishawishi na vikwazo viko tu na vinashamiri kila siku....kusema ndoa za siku hizi zimejaa unafiki,sijui ni za siku zipi ambazo hazikuwa na unafiki......manake kukiuka viapo vya ndoa ni kitu kimekuwepo tangu enzi hizo...mapungufu ya kwenye ndoa si unafiki,ni matokeo ya kuishi binadamu wawili ambao wote wamepungukiwa utukufu wa Mungu na wana tamaa...

Sijidanganyi wala simdanganyi muumba wangu anayeona sirini kwa kupinga kuishi pamoja kabla ya ndoa....kutokuishi pamoja kabla ya ndoa hakunifanyi mimi/wala yeyote mkamilifu ila nina sina budi kujitahidi kadri ya uwezo wangu kutii na kufuata taratibu za dini ninayoiabudu....na tamaduni nilizolelewa....
 


Well said mamito nimeipenda hii, hata mimi baba nyanzala analijua kabisa, namwambiaga fanya vyote ila mwanangu tafa.................
 
Ukiliangali hili swala ki-ivyo kweli hutauona umuhimu wa ndoa tena,atleast kwa hizi ndoa za siku hizi zilizojaa usanii.
Lakini kama Nyamayao alivyosema hapo juu,hata iyo ya kuishi bila ndoa itafika time mnafamilia na mtahesabika kuwa mume na mke.so hata kama hukufunga ndoa and now you have your two kids with this guy na ameanza ushenzi,lets say ni after 10 years...dont you think walking out of this 'staying together' thing wont be as hard as it is in official marrieges?
Mi naona yote yaleyale tu,omba Mungu ukupe mume/mke mwema ili muishi vyema kwa amani forever iwe ndoani au 'stay together'
 
aaaaahhh Lizzy watoto wa watu?? wakina na nani? wanaume? subutu yake!!!!!!!

ngoja nitoke maana naona nataka kuwaka!!!

Susy bwana....wamekufanya nini tena hawa wandugu??Mwenyewe kuna mmoja sio kabisa ila bado naamini wenzake sio wale wale!!!
Alafu hilo chozi silifurahii kabisaaaaaaa!!
 

Hili neno sweetness
coz unaweza kuwa kwenye hiyo ndoa lakini unayoyafanya ni aibu mbele za Mungu na binadamu wenzio
 
mimi naamini ukipata ubavu wako ambao mungu ndio aliokupangia, hata awe na tabia zipi au mpate misuko suko vipi mtaishi mpaka kifo kiwatenganishe. Tatizo ndoa za siku hizi ni za kulazimisha

Hapo kwenye red umemaliza kabisaaaa mpendwa!
 

Hehhehe nimekusoma sasa....

Ahh kwa watoto wako inabidi uwe mkali mpendwa...hamna zaidi yao.
Alafu unajua ''wavumiliaji'' wa muda mrefu wengi wao hua wanawatumia watoto kama sababu tu ila ukweli ni kwamba hua hawafanyi kwaajili ya watoto ila kwaajili yao binafsi??Imagine mtoto anaposhuhudia mama na baba wakigombana kila leo...baba akileta mwanamke ndani au amempa dada mimba...baba akimpiga mama au hata na watoto huyo mtu anakua amesaidia vipi watoto??Mi hua naona ni ubinafsi tu tusiotaka kuukubali hivyo tunatumia watu wengine kusema navumilia kwaajili yenu....kumbe wao ndo wanavumilia kwaajili yako!
 
Ya yule mtu muache kama alivyo mara yes mara no si ndo kama hivyo tena unajua bana acha kunivizia.

Hili linahitaji niwe nimetulia sana nitapost nikiwa home nimetulia

Hahahahah....alafu hawachoki kuimba kwamba sis wanawake ndo watu wa ndio hapana...ngoja nimpotezee!!!Haya dear nasubiria ukishapumzika na kikombe chako cha kahawa umwage busara zako kwa uchache hapa!!
 
Haya ni mashindano mabaya mno; Wanawake siku hizi(ya zamani sina hakika) wanashambulia wanaume kuwa ndio chanzo cha ndoa kuvurugika, na wanaume wanasema nijeuri ya wanawake baada ya kupewa uhuru na kuwa na kipato wameota mapembe, sasa mwisho wa siku ni kupotea/kutoweka kwa familia!

Lakini Mungu hawezi kosa watu wake, lazima watakuwepo watu ambao wataishi kwa ndoa na kwa amani kama inavyotakiwa kiimani. Na wengine wataendelea na mbwembwe zao za kuingia katika ndoa na kutoka, mwisho wa maisha ana msururu wa wenza wawe wa ndoa au wa kuishi pamoja........
 
penye red nakupinga 100% tukiendekeza hayo mtakuja kukuta ndugu wanaoana,wakina mama kuwezeshwa hakumaanishi usiolewe,na hii naungana na wazee wa zamani kuwa mtoto wakike asisome,maana sasa hivi wamesoma na kupata kazi anataka wazae hovyo kisa anauwezo wa kulea hii ni hatari sana,cha msingi ni hivi semeni hamtaki kuolewa na msiwe na familia,
 
tukiendekeza hayo mtakuja kukuta ndugu wanaoana,wakina mama kuwezeshwa hakumaanishi usiolewe,na hii naungana na wazee wa zamani kuwa mtoto wakike asisome.
Kwahiyo na wanaotaabika waendelee kung'ang'ana na ndoa kwaajili ya watoto tu eh?Alafu waishie kutaabisha na hao watoto!?Kuhusu ndugu kuoana kwani kuna wanaume wangapi wanaozaa nje ya ndoa zao alafu baadae watoto wa huyo huyo mwanaume wanaletana nyumbani kama wapenzi/wachumba watarajiwa?
 
Badala utusaidie mawazo ili na sie tuongeze...

Ushasaidiwa kwa swali litakaloamsha fikra na majadiliano, ili kuweza kujadili vizuri hili swala inabidi kuelewa ndoa ni nini.

Kama huelewi ndoa ni nini, au kama kuna watu tofauti wanaangalia ndoa kwa mitazamo tofauti, tunaweza kushindwa kuelewana bila kuelewa sababu.

Ndiyo maana hili swali ni muhimu sana.
 

Mimi sielewi au labda sijui...naomba unisaidie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…