Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Wakuu nimejaribu kutafuta contact za Fair Competition Commission (FCC) ili niweze kuishitaki kampuni ya Star Media Ltd maarufu kama Star Times kwa kutangaza bei ya bidhaa ambayo ni tofauti na ile wanayotoza. Ikumbukwe kuwa Star Media ni moja kati ya kampuni tatu zilizopewa zabuni ya kuuza ving'amuzi kwa ajili ya migration from analogue to digital broadcasting. Kampuni nyingine ni Agape Associates Limited and Basic Transmissions Limited.
Hawa jamaa wamekuwa wakitangaza bei ya king'amuzi kimoja kuwa ni "sh. 39,000/= tu"!. Lakini ukienda katika shop/branch zao popote pale Dar es Salaam wanakuambia yafuatayo:
Sasa mimi ninatamani niyafikishe mambo yote haya katika Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC), lakini nimesearch website yao nipate contacts bila mafanikio. Anayewajua hawa jamaa wa FCC aniwekee hapa phyisical contacts niwashitaki Star Times. Nadhani nitakuwa nimewajibika kwa upande wangu kuliko kulalamika tu.
Hawa jamaa wamekuwa wakitangaza bei ya king'amuzi kimoja kuwa ni "sh. 39,000/= tu"!. Lakini ukienda katika shop/branch zao popote pale Dar es Salaam wanakuambia yafuatayo:
- Kwamba huwezi kununua king'amuzi bila ya kifurushi (ambacho kidogo sana kinauzwa sh. 9,000/=, kwa hiyo pamoja na king'amuzi minimum jumla unatakiwa kutoa sh. 48,000/= na sio 39,000/= wanayotangaza
- Kama vile haitoshi, kila shop yao utapewa jibu la kwamba kifurushi cha sh. 9,000/= kimeisha, so walau ununue kinachofuata kwa unafuu wa bei kinachouzwa sh. 18,000/= kwa hiyo pamoja na king'amuzi jumla unatakiwa utoe sh. 57,000/= na sio 39,000/= wanayotangaza.
- Hawatangazi kuwa unatakiwa ununue antenna yao ili ukamate vizuri signal, lakini ukifika katika shop yao ndio unakutana na vitisho hivyo kuwa signal inaweza kuwa weak kwa kuwa hukutumia antenna yao, so unalazimika kununua.