Kuitwa kwenye usaili baada ya kupangiwa kituo cha kazi

SemeniAbdallah

New Member
Joined
Mar 7, 2025
Posts
4
Reaction score
3
Habari, mimi ni binti ambaye niliomba ajira serikalini mwaka jana sehemu mbili (Taasisi A, na Taasisi B) kupitia utumishi na nikafanikiwa kupata na kupangiwa kazi kwenye Taasisi A. Hadi sasa nina miezi minne kazini na nimeshapata cheki namba.

Taasisi B ilikuwa bado haijaita watu kwenye usaili, wiki hii majina ya kuitwa kwenye usaili ya Taasisi B yametoka na jina langu lipo. Na kutokana na taarifa mbalimbali inaonekana maslahi ya Taasisi B ni mazuri kuliko Taasis A.

Nimekuwa na maswali haya;

1. Je, niende kwenye usaili wa Taasisi B?
2. Endapo nikafaulu hatua ya mchujo (kuandika) na ya kuongea na kupata nafasi Taasisi B itakuwa rahisi kuhama?
3. Taasisi A hawataleta shida kwenye uhamisho?
4. Hadi sasa bado sijathibitishwa kazini, je hii haitaleta shida kazini (kimaadili) endapo Taasisi niliyopo sasa ikakataa kuniruhusu?

Natanguliza shukrani zenu.
 
Ukishapata cheki Na. Lazima ufuate taratibu za utumishi kufanya sahili kwenye taasisi nyingine, kwasasa huna sifa lazima uthibitishwe then ukae kituo cha sasa miaka mitatu. Ukiamua kwenda tu hata ukipata hiyo nafasi utarudishwa huko ulipopata cheki namba sasa
Nashukuru kwa taarifa.
 
Kama umeshapata check number, basi tuliza wowowo hapo ulipo.... Bado hauna sifa za kuweza kwenda kufanya interview huko.
 
Unahama hakuna kinachoshindikana, shida wengi huogopa na HR wengi ni wanonko hawataki kuachia watu waondoke.
 
Labda kama taasisi B ni private au mashirika ya umma ila kama local government na serikali kuu ilo haliwezekani.
 
Habari, mimi ni binti ambaye niliomba ajira serikalini mwaka jana sehemu mbili (Taasisi A, na Taasisi B) kupitia utumishi na nikafanikiwa kupata na kupangiwa kazi kwenye Taasisi A. Hadi sasa nina miezi minne kazini na nimeshapata cheki namba.

Taasisi B ilikuwa bado haijaita watu kwenye usaili, wiki hii majina ya kuitwa kwenye usaili ya Taasisi B yametoka na jina langu lipo. Na kutokana na taarifa mbalimbali inaonekana maslahi ya Taasisi B ni mazuri kuliko Taasis A.

Nimekuwa na maswali haya;

1. Je, niende kwenye usaili wa Taasisi B?
2. Endapo nikafaulu hatua ya mchujo (kuandika) na ya kuongea na kupata nafasi Taasisi B itakuwa rahisi kuhama?
3. Taasisi A hawataleta shida kwenye uhamisho?
4. Hadi sasa bado sijathibitishwa kazini, je hii haitaleta shida kazini (kimaadili) endapo Taasisi niliyopo sasa ikakataa kuniruhusu?

Natanguliza shukrani zenu.
Tulia binti kutofautiana maslahi nikawaida tu, hata ukienda uko na ukapata nako baada ya muda utasikia kwingine kwenye maslahi zaidi
 
Back
Top Bottom