KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Huu uzi niwakuwachana wana JamiiForums haswa wale ndakindaki wa jukwaa la siasa.
Niseme tu ukweli kushadadia kuteuliwa ama kutenguliwa kwa baadhi ya watu, humu ndani imekuwa ndio mada zinazo tambaa kwasasa. Naweza kuita ni ujinga, upuuzi ama ni uzwazwa.
jukwaa hili halifai kuendekeza mijadala ya namna hiyo, inaonekana tu wepesi sana na michezo ya kisiasa tunajadili sahivi kutenguliwa kwa watu fulanifulani tunasahau wanaweza kuteuliwa tena! Mbona tupo wepesi sana kuhadaika!
Ni kweli tunachokihitaji kwenye nchi yetu ni kuteuliwa ama kutenguliwa ama kutimiziwa matakwa yetu katika nchi? Kwanini tunapenda sana habari za kidakudaku kushindwa zile zenye maana sana.
Mijadala iliyokuwa inatakiwa kutamba sasahivi ni namna gani hizo idara zinaweza kuleta tija zaidi, wapi walifaulu waliotoka na wapi walifeli lakini ni tofauti kabisa sioni utofauti na wapenda udaku!
Hii ni sehemu nyeti jitahidini kubadirika mvue hilo likaptura. JamiiForums inaweza kuwa dira nzuri sana maneno mnayo andika yanaweza kuwa dira yenye mwanga ktk nchi, kuliko kuhadaika na mitego midogo midogo yakisiasa!
Kwanza mi naona hizo njemba zimepumzishwa tu kwa kazi ya 2025 ikimalizika zitarudishwa nothing more!