Kujali kunaanza na wewe kujijali kwanza

Kujali kunaanza na wewe kujijali kwanza

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
KUJIONA | KUJIPENDA | KUJIJALI

Jambo lolote unalohisi haupewi ni kwa sababu hauna, ukiona mtu analalamika hapendwi ndani yake yeye ndio upendo hamna, mtu akisema anadharauliwa ndani yake dharau zimejaa, vivyo hivyo kwa kupoteza kipaumbele chako mwenyewe.

Hii ni kwa sababu ukiwa na kitu ndani yako hata kama nje kikikosekana bado unaouwezo wa kukitengeneza, mtu mwenye upendo hata usipompenda haiwi sababu ya yeye kutokukupenda, na upendo uko ndani ya mtu sio kwa kudhihirishwa na vitu vya nje, mtu akisema anadharauliwa tambua kaanza kujidharau yeye ndio maana kaona anadharauliwa, mapokeo na matokeo yanategemea sana ujazo wako ndani, mtu anaweza kukuonyesha tabia za dharau na ukamuonyesha heshima akajifunza kutoka kwako, lakini ikiwa ndani yako umezijaza utaona umeguswa sana na umeonewa sana.

Hivyo tabia na mwenendo wote mzuri ili kuustawisha anza kwa kujifanyia mwenyewe, Jione kuwa ni wa thamani ili uweze kuiona thamani ya mwenzako, Jipende kwanza wewe ili ujue umuhimu wa kumpenda mwingine, jijali wewe ili uone kwanini unatakiwa kuwajali wengine. Mambo na vitu vianzie ndani kwako kwako ndio viende nje kwa wengine.

ANZA LEO KUTENGENEZA UBORA WAKO ILI UWABORESHE NA WENGINE.

Maisha ni haya haya wa kubadilika ni wewe…..

Elisha Chuma ©️echu

————- www.echu.co.tz —————

Septemba Quotes.zip - 8.png
 
Back
Top Bottom