Kwema wazee, Kwa knowleldge ndogo ambayo ninayo mimi.
Kinachobeba mzigo kwenye tairi ni Upepo.
Logic ya kujaza nyuma upepo (PSI) kubwa ni kwa ajili ya kuhandle mzigo. Hii hua inafanyika zaidi kwenye magari ya mizigo. Standard PSI kwa passenger cars ni 35bars, Lakini wengine hueka 40 kwa sababu unakuta anabeba mizigo ili hata ikipungua inarange na tairi za mbele. Lakini Kitalaam kwa Passenger cars hizi ni vyema ukaweka PSI moja tairi zote Nne.
Pia kuhusu Kufanya rotation ya matairi kwenye gari, Magari mengi (2wheel) yanavutia mbele hivyo husababisha tairi za mbele kuisha haraka zaidi kwa sababu ya traction kati yake na barabara. Lakini pia kiusalama tairi za mbele ndio zinatakiwa kua imara zaidi kwa sababu zile ndio zinasaidia kwenye uelekeo wa gari(Rotation), Endapo ikapasuka tairi ya mbele ukiwa kwenye high speed unahatari zaidi ya kupata ajali mbaya kuliko ile ya nyuma ambayo haizunguki kulia na kushoto(Rotation). Hivyo Basi kitalaam ili tairi zote ziishe kwa uwiano sawa na ziwe salama atleast kila baada ya km5000 unafanya rotation, either za mbele kwenda nyuma na nyuma mbele, au unafanya full circle rotation ambayo kila tairi inahama kwenda kwa mwingine mpaka spare tire.