Kujaza wanasiasa uwanjani ni mkosi kwa timu ya Taifa

Kujaza wanasiasa uwanjani ni mkosi kwa timu ya Taifa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Timu hii ikifanya vibaya inakuwa ya Wananchi lakini ikishinda kagemu kamoja au tuwili inakuwa ya Viongozi.

Sasa matokeo yake ndio kama mlivyosikia, eti viongozi wasio na upendo wowote na timu wala wachezaji leo wanajifanya ndio wenye timu!

Msipojirekebisha mtaishia kuwa Kichwa cha Mwendawazimu tu.
 
Na taa zikazima ghafla, aisee bongo bahati mbaya
Taa zimezimwa na wao wenyewe uwanjani hazikujizima! Mchina hakosei kiboya!

Hivi lini we uliona taa zimezingua kwa Mpalanger ( sorry kwa Mkapa ) mechi Gani? Lini? Itaje!

Jana Taifa la Tanzania limeaibika sana duniani kote nchi ya hovyo kabisa japo sisi ni donor country tuna uwezo kutoa pesa mabilioni kusaidia matajiri kina Osman Bey wa Turkey na maskini waMalawi ila taa za uwanja mmoja tu tumeshindwa!!

Viongozi wetu wengi ni vilaza hivi hawakukagua taa? kazi wanayoimudu ni kusimamia manunuzi ya vifaa vya amrisha tu maafande kupiga waandamanaji ila mengine hawana faida!

Hata taa za uwanja mmoja tu nazo tumeshindwa? Kweli tuna Waziri wa umeme? Saa ingine kipara hakina faida.

Haya kipi tunaweza?

Ndege ZZK anadai zimepaki, mwendokasi tumeshindwa, elimu tumeshindwa, ajira tumeshindwa, English speaking tumeshindwa, Kilimo tumeshindwa, SGR tumeshindwa tunasuasua, Bwawa la Nyerere tumeshindwa kujaza maji Toka Lake Victoria!! Boli tumeshindwa, Kweli bongo akili hatuna, viongozi bomu tu!

Tunayoweza
1.Ufisadi
2.Massage
3.Kuiba wake na waume za watu
4 Urasimu
5 uoñgo, umbea na majungu

Tumefanikiwa Royal Tour basi!
But hongera Bimkubwa for free tickets
 
Back
Top Bottom