''Kujazia'' ball joint, rack end clutch plate na brake shoe

Rohombaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
13,067
Reaction score
10,393
Wadau,
Nimepita mahali nikaona wanafanya hii shughuli ya kuzirudisha upya vipuri vya magari.
Vipi kuhusu uimara wa gari na usalama wa mtumiaji baada ya kufanya hivi?
Wazoefu naomba mnijuze tafadhali
 
Vinadumu ila sikushauri. Heri ujichange ununue kipya maana bei zake siyo kubwa. Mara nyingi wanaonunua ni wale vishoka wanaotumwa na matajiri kwenda kufanyia service magari
 
Dah...ahsante chief... swali langu hasa lillilenga kwenye uimara wa gari na usalama wa mtumiaji...Vipi kuhusu usalama wa mtumiaji? maana vipuri vyenyewe vinahusu sana udhibiti wa mwendo na muelekeo wa gari..
 
Ndiyo maana nikakwambia ni vizuri ukinunua vipya. Wanaonunua ni wale ambao hawaangalii madhara yatakayoweza kutokea mbele. Pia kudumu kwa kifaa inategemea na utunzaji ingawaje hivyo vya kujazia hawakupi guarantee halisi zaidi ya kukwambia kitadumu ila kama mfuko umepwaya unaweza kuweka kwa matarajio ya kubadilisha baada ya muda mfupi. Hivyo huwa nasema havitofautiani na tairi used ambazo uhakika wa kudumu huwa mdogo
 
Dah..Ahsante kwa elimu mujarab..Kipi hasa kinachofanyika ''kujazia'' kwenye ball joint iliyochoka?... Nimejaribu kuitafuta hii teknolojia lakini sijaionana popote...na nilipita wanapoifanya hii kazi lakini hawakutaka kabisa nijue kinachofanyika wakati wa kujazia...
 
Wanachofanya ni kuchoma gololi ya ndani ili kuongezea ukubwa au wanaweza kuipiga spot na hivyo kwa mwonekano wa nje huwezi kuona play iliyokuwepo na muda mwingine wanachomea nyumba ya hiyo gololi ambapo kinadharia hizo haziwezi kudumu kwa muda mrefu kutokana na zilivyokwisha tengenezwa
 
Attachments

  • Screenshot_2016-11-15-10-29-17.png
    Screenshot_2016-11-15-10-29-17.png
    74.1 KB · Views: 103
Wanachofanya ni kuchoma gololi ya ndani ili kuongezea ukubwa au wanaweza kuipiga spot na hivyo kwa mwonekano wa nje huwezi kuona play iliyokuwepo na muda mwingine wanachomea nyumba ya hiyo gololi ambapo kinadharia hizo haziwezi kudumu kwa muda mrefu kutokana na zilivyokwisha tengenezwa
Dah. Ahsante kwa ilm
 
Back
Top Bottom