Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za asubuhi;
Kama kawaida huwa kuna maamuzi mengi magumu ya kufanya katika maisha,baadhi yake ikiwa ni uamuzi wa ama kujiajiri au kuajiriwa.
Uamuzi au uchaguzi huu mara nyingi haufanywi na mtu kwa hiari yake bale husukumwa na circumstance pamoja na fursa.Wengi wa waliojariwa ni kwa sababu waliomba ajira wakapata na wengi ambao hawajaajiriwa ni kwa sababu ama hawakupata ajira au walipa fursa.
Vyovyote vile uamuzi wowote huwa na msukumo bila kujali uwezo binafsi wa mtu.
Ni ukweli usiopingika kwamba kama utaajiriwa au kujiajiri bado ugumu utakua pale pale na usifikiri kwamba ugumu ulioko kwenye kujiajiri basi utaondoka pale ukiajiriwa au ugumu ulioko kwenye kuajiriwa utaondokana nao ukijiajiri hapana.Changamoto na zile zile.
Tofauti kati ya kuajiriwa ama kujiajiri ni ndogo sana na kwamba vyovyote utakavyochagua kuna kanuni za msingi zitakufunga.Baadhi ya kanuni hizi ni bidii,ubunifu,uvumilivu.Zinahitajika katika ajira na kujiajri na ni msingi wa mafanikio.
Unapojiajiri,utafanya kazi overtime lakini hutadai malipo ya overtime,ili ukipiga faida kubwa ni yako yote.Ukiajiriwa utalipwa overtime ila ukizalisha faida kubwa utakula ujira wako tu.
Ukijiajir jiandae pia kuajiri watu kama kweli unataka kukua kibiashara.Unapoajiri watu tambua kwamba baadhi yao watakuwa na fikra kama zako,na ndoto za kujiajiri hivyo waheshimu sana.
Ukiajiri muheshimu sana boss wako na ufanye kazi kwa bidii kwani itakujengea nidhamu na kukuwezesha kumudu kazi zako pindi uamuapo kujiajiri.
Usikimbilia kujiajri kama wewe ni mvivu asiyekuwa na nidhamu ya kazi.Usikimbilie kujiajiri kama hujaona fursa ya uhakika,Usikimbilie kujiajiri kama hujajianda kubadili kabisa mfumo wako wa maisha.Kujiajiri sio kichaka cha watu wavivu na wazembe.
Yote kwa yote,Iwapo kwa sababu yoyote ile umeamua au kulazimik kujiajiri au kuajiriwa basi fahamu kuwa msingi wa mafanikio yako ni Nidhamu,bidii na uvumilivu bila kusahau ubunifu.
Uwe na wakati mwema